Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yer 23

23
Kurejeshwa toka Uhamishoni
1 # Yn 10:10-12; Zek 11:5-7,15-17 Ole wao wachungaji, wanaoharibu kondoo za malisho yangu na kuwatawanya! Asema BWANA. 2#Kut 32:34Kwa sababu hiyo BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, juu ya wachungaji wanaowalisha watu wangu, Mmetawanya kundi langu, na kuwafukuza, wala hamkwenda kuwatazama; angalieni, nitawapatiliza uovu wa matendo yenu, asema BWANA. 3#Yer 32:37Nami nitakusanya mabaki ya kundi langu, katika nchi zile zote nilizowafukuza, nami nitawaleta tena mazizini mwao; nao watazaa na kuongezeka. 4Nami nitaweka juu yao wachungaji watakaowalisha; wala hawataona hofu tena, wala kufadhaika, wala hatapotea hata mmoja wao, asema BWANA.
Chipukizi la Haki la Daudi
5 # Isa 4:2; 11:1; 32:1; Yer 33:14; Dan 9:24; Zab 72:2 Tazama siku zinakuja, asema BWANA, nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atamiliki mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika nchi. 6#Kum 33:28; Zek 14:11; Yer 33:16; 1 Kor 1:30Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli atakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, BWANA ni haki yetu. 7Kwa hiyo, angalia, siku zinakuja, asema BWANA, ambapo hawatasema tena, Aishivyo BWANA, aliyewatoa wana wa Israeli katika nchi ya Misri; 8#Isa 43:5lakini, Aishivyo BWANA, aliyewapandisha na kuwaongoza wazao wa nyumba ya Israeli kutoka nchi ya kaskazini, na kutoka nchi zote nilikowafukuza; nao watakaa katika nchi yao wenyewe.
Manabii wa Uongo Wanaoahidi Tumaini Washutumiwa
9 # Hab 3:15 Katika habari za manabii.
Moyo wangu ndani yangu umevunjika,
Mifupa yangu yote inatikisika.
Nimekuwa kama mtu aliye mlevi,
Na kama mtu aliyeshindwa na divai;
kwa ajili ya BWANA, na kwa ajili ya maneno yake matakatifu.
10 # Hos 4:2 Maana nchi imejaa wazinzi; kwa sababu ya kuapa nchi inaomboleza; malisho ya nyikani yamekauka; mwenendo wao ni mbaya, na nguvu zao si za haki. 11#Sef 3:4; Eze 8:11#Mit 4:19Maana nabii, na kuhani, wote wawili wanakufuru; naam, katika nyumba yangu nimeuona uovu wao, asema BWANA. 12Kwa ajili ya hayo njia yao itakuwa kwao kama mahali pa kuteleza gizani; watatelemshwa na kuanguka hapo; kwa maana nitaleta uovu juu yao, naam, mwaka wa kujiliwa kwao, asema BWANA. 13#1 Fal 18:18; Isa 9:16Nami nimeona upumbavu katika manabii wa Samaria; walitabiri kwa Baali, wakawakosesha watu wangu Israeli. 14#Eze 13:22; Isa 1:9; Mwa 18:20; Eze 16:49Katika manabii wa Yerusalemu nimeona neno linalochukiza sana; hufanya zinaa; huenenda katika maneno ya uongo, hutia nguvu mikono ya watendao maovu, hata ikawa hapana mtu arejeaye na kuuacha uovu wake; wote pia wamekuwa kama Sodoma kwangu, na wenyeji wake kama Gomora.
15Basi BWANA wa majeshi asema hivi, katika habari ya manabii, Tazama, nitawalisha pakanga, nitawanywesha maji ya uchungu; kwa kuwa kutoka kwa manabii hao wa Yerusalemu kukufuru kumeingia katika nchi yote. 16#Mit 19:27; Mt 7:15BWANA wa majeshi asema hivi, Msisikilize maneno ya manabii wakiwatabiria; huwafundisha ubatili; hunena maono ya mioyo yao wenyewe; hayakutoka katika kinywa cha BWANA. 17#Zek 10:2; Mik 3:11Daima huwaambia wao wanaonidharau, BWANA amesema, Mtakuwa na amani; nao humwambia kila mtu aendaye kwa ukaidi wa moyo wake, Hamtapatwa na ubaya wo wote. 18#Ayu 15:8; 1 Kor 2:16Maana, ni nani aliyesimama katika baraza la BWANA, hata akalifahamu neno lake na kulisikia? Ni nani aliyelitia moyoni neno langu, na kulisikia? 19#Yer 25:32Tazama, tufani ya BWANA, yaani, ghadhabu yake, imetokea; ni dhoruba ya kisulisuli; itapasuka, na kuwaangukia waovu vichwani. 20#2 Fal 23:26,27; Mwa 49:1Hasira ya BWANA haitarudi, hata atakapokwisha kuyatimiza makusudi ya moyo wake; katika siku za mwisho mtalifahamu neno hili kabisa. 21Mimi sikuwatuma manabii hao, lakini walikwenda mbio; sikusema nao, lakini walitabiri. 22Lakini kama wangalisimama katika baraza yangu, ndipo wangaliwasikizisha watu wangu maneno yangu, na kuwageuza waziache njia zao mbaya, na uovu wa matendo yao. 23#1 Fal 20:23,28; Zab 113:6Mimi ni Mungu aliye karibu, asema BWANA, mimi si Mungu aliye mbali. 24#Zab 11:4; 139:7; Amo 9:2; Ebr 4:13; 1 Fal 8:27; 2 Nya 2:6; Isa 66:1Je, mtu ye yote aweza kujificha mahali pa siri, nisimwone? Asema BWANA. Je! Mbingu na nchi hazikujawa nami? Asema BWANA. 25#Ebr 4:13Nimesikia waliyoyasema manabii wanaotabiri uongo kwa jina langu, wakisema, Nimeota ndoto; nimeota ndoto. 26Je! Mambo hayo yatakuwa katika mioyo ya manabii wanaotabiri uongo hata lini, manabii hao wenye udanganyifu katika mioyo yao wenyewe? 27#Kum 13:11; Mdo 13:8; 2 Tim 3:6-8; Amu 3:7Wanaodhania ya kuwa watawasahaulisha watu wangu jina langu kwa ndoto zao, wanazomhadithia kila mtu jirani yake, kama vile baba zao walivyolisahau jina langu, kwa ajili ya Baali. 28#2 Kor 2:17; 1 Pet 4:10Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na neno langu, na aseme neno langu kwa uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko ngano? Asema BWANA. 29Je! Neno langu si kama moto? Asema BWANA; na kama nyundo ivunjayo mawe vipande vipande?
30 # Kum 18:20; Yer 14:14,15 Basi kwa sababu hiyo mimi ni juu ya manabii hao, asema BWANA, wanaompokonya kila mtu jirani yake maneno yangu. 31Tazama, mimi ni juu ya manabii, asema BWANA, wanaotumia ndimi zao na kusema, Yeye asema, 32#Sef 3:4Tazama, mimi ni juu ya hao wanaotabiri ndoto za uongo, asema BWANA, na kuzisema, na kuwakosesha watu wangu kwa uongo wao, na kwa majivuno yao ya upuzi, lakini mimi sikuwatuma, wala sikuwapa amri; wala hawatawafaidia watu hawa hata kidogo, asema BWANA. 33#Isa 13:1; Yer 17:15; Mal 1:1Na watu hawa, au nabii au kuhani, atakapokuuliza, akisema, Mzigo wa BWANA ni nini? Ndipo utawaambia, Mzigo gani? BWANA asema, Nitawatupilia mbali. 34Na katika habari ya nabii, na kuhani, na watu, watakaosema, Mzigo wa BWANA, mimi nitamwadhibu mtu yule, na nyumba yake. 35Mtasema hivi kila mtu na jirani yake, na kila mtu na ndugu yake, BWANA amejibu mtu? Na, BWANA amesemaje? 36#Mt 12:36; Mdo 13:10,11; Gal 1:7,8Na mzigo wa BWANA hamtautaja tena; maana neno la kila mtu ndilo litakalokuwa mzigo wake; maana ninyi mmeyapotosha maneno ya Mungu aliye hai, ya BWANA wa majeshi, Mungu wetu. 37Nawe utamwambia nabii hivi, BWANA amekujibu nini? Na, BWANA amesemaje? 38Lakini mkisema, Mzigo wa BWANA, basi, BWANA asema hivi, Kwa sababu mwasema neno hili, “Mzigo wa BWANA”; nami nimemtuma mtu kwenu kusema, Msiseme, “Mzigo wa BWANA”; 39#Kum 31:17,18; Hos 4:6basi, kwa hiyo angalieni, nitawasahau ninyi kabisa, nami nitawatupilia mbali, pamoja na mji huu niliowapa ninyi na baba zenu, mtoke mbele za uso wangu; 40#Yer 20:11; Dan 9:16nami nitaleta juu yenu aibu ya milele, na fedheha ya daima, ambayo haitasahauliwa.

Iliyochaguliwa sasa

Yer 23: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha