Yeremia 23:34-35
Yeremia 23:34-35 Biblia Habari Njema (BHN)
Tena nabii au kuhani, au mtu yeyote atakayesema ‘Mzigo wa Mwenyezi-Mungu,’ nitamwadhibu pamoja na jamaa yake yote. Kitu mnachopaswa kuulizana nyinyi kwa nyinyi ni ‘Mwenyezi-Mungu amejibu nini?’ au, ‘Mwenyezi-Mungu amesema nini?’
Yeremia 23:34-35 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na katika habari ya nabii, na kuhani, na watu, watakaosema, Mzigo wa BWANA, mimi nitamwadhibu mtu yule, na nyumba yake. Mtasema hivi kila mtu na jirani yake, na kila mtu na ndugu yake, BWANA amejibu mtu? Na, BWANA amesemaje?
Yeremia 23:34-35 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)