Matendo 23:12-13
Matendo 23:12-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Kulipokucha, Wayahudi walifanya kikao cha faragha. Wakala kiapo: “Hatutakula wala kunywa mpaka tutakapokuwa tumekwisha muua Paulo.” Watu zaidi ya arubaini ndio waliokula njama kufanya hivyo.
Shirikisha
Soma Matendo 23Matendo 23:12-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kulipopambazuka, Wayahudi wakafanya mapatano, wakajifunga kwa kiapo kwamba hawatakula wala hawatakunywa hadi wamwue Paulo. Na hao walioapiana hivyo walikuwa zaidi ya watu arubaini.
Shirikisha
Soma Matendo 23