1 Wafalme 6:29-30
1 Wafalme 6:29-30 Biblia Habari Njema (BHN)
Kuta za kila chumba alizipamba kwa kuchongwa michoro ya viumbe wenye mabawa, mitende na michoro ya maua yaliyochanua. Aliipaka dhahabu sakafu ya vyumba vya ndani na vya nje.
1 Wafalme 6:29-30 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Akazinakshi kuta zote za nyumba kwa nakshi za makerubi, na mitende, na maua yaliyofunuka wazi, pande za ndani na nje. Na sakafu ya nyumba akaifunika na dhahabu ndani na nje.
1 Wafalme 6:29-30 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Akazinakshi kuta zote za nyumba kwa nakshi za makerubi, na mitende, na maua yaliyofunuka wazi, pande za ndani na nje. Na sakafu ya nyumba akaifunika na dhahabu ndani na nje.
1 Wafalme 6:29-30 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Juu ya kuta zote zilizozunguka Hekalu, za vyumba vya ndani na vya nje, zilipambwa kwa nakshi zilizokatwa za makerubi, miti ya mitende na maua yaliyochanua. Pia alifunika sakafu zote za vyumba vya ndani na vya nje vya Hekalu kwa dhahabu.