Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kutorokea MisriMfano

Kutorokea Misri

SIKU 4 YA 7

Kupigana na dhambi

Misri inaweza kuwa pahali pa kutorokea wakati wa shida. Lakini pia misri yaweza kuwa mfano wa kurudi kataika maisha ya dhambi. Mara nyingi tunapata kuwa wakristo wanakuwa na nguvu ya kiroho, lakini kwa wengi, hiyo haidumu sana. Wasipo na imani ya kutosha huwa wanarudi katakia maisha ya dhambi waliokuwa wakiishi kabla ya wokovu. Na hii inakuwa kawaida kwa wengi. Kuwa na nguvu halafu punde si punde kuteleza tena. 

Kama tu wana wa Israeli walipokuwa wafungwa misri, dhambi hutufanya kuwa wafungwa na kila mara tunapojaribu kuepuka, watawala wa watumwa hutulazimu tuishi katika hiyo hali.

Katika somo la leo cha Zaburi 18:2, tunapata kuwa kuna matumaini ya kuepuka maisha ya dhambi, kwani Bwana ndiye pekee yeye anayeweza kutukomboa kutoka katika maisha ya dhambi kwani yeye ndiye mwamba wa ukombozi wetu.  

Ombi la leo ni Bwana kutusaidia ili tugundue ya kwamba ni yeye peke anaye uwezo wa kutukomboa kutoka kwa maisha ya ufungwa misri.

 

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Kutorokea Misri

Muda mfupi baada ya ziara ya Wayahudi, ambao walijua kwamba Mfalme Herode alitaka kuua watoto wa eneo hilo, malaika alimtokea Yosefu katika ndoto kumwambia aende Misri na Maria na mtoto wa kijana Yesu. Swali 1: Ni nini u...

More

Tungependa kushukuru GNPI Kenya kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.gnpi-africa.org

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha