Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Neno Moja Litakalobadilisha Maisha YakoMfano

One Word That Will Change Your Life

SIKU 3 YA 4

Mchakato wa Neno Moja





Weka


Licha ya utangazaji wote, bado tunapenda ukweli kwamba Mwaka Mpya ni fursa ya kusafisha mabaya yote na kuanza upya. Tuna uhuru wa kupoteza kilo fulani za uzani wetu, kujitolea kwa ibada ya kila siku, kushinda michezo mingi, kufanya mazoezi kwa nguvu, kuomba kwa imani zaidi, kutumia wakati wetu mwingi na familia, kulipa bili, kuongeza masomo au hata kujumuika pamoja kwa ajili ya Yesu Kristo na marafiki. Lakini ukweli ni kwamba orodha hiyo ndefu ya maazimio ni nadra sana yaafikiwe.





Suluhisho moja ni kutupilia mbali orodha hiyo na kubaki na neno moja muhimu kwa mwaka ujao, kulifanya kuwa rahisi na la kimsingi.





Kwa hivyo, hembu sasa tuelekee upande wa vitendo wa dhana ya mada ya Neno Moja. Hizi hapa ni hatua za kukusaidia kugudua mada yako ya Neno Moja. Weka akilini kuwa mchakato huu utachukua muda, lakini ni wa thamani. Kama wewe ni mwanamichezo, kocha, mzazi au kiongozi wa biashara, mchakato huu unaweza kuletea mafanikio katika kila eneo la maisha yako.





Mchakato wa Neno Moja una hatua tatu rahisi – Tazama Ndani, Tazama Juu na Tazama Nje.





Hatua ya Kwanza – Tayarisha Moyo Wako (Tazama Ndani) – Hapa ndipo unachukua hatua ya kujitoa kwa kasi ya kukera, makelele na machafuko. Kutafuta kuwa peke yako na kuwa kimya kunaweza kuwa kibarua kigumu, lakini kusikia kutoka kwa Mungu ni muhimu. Tunapomuacha Mungu achunguze mioyo yetu, atatupatia uwazi.





Hatua ya 2 – Gundua Neno Lako (Tazama Juu) – Hatua hii hutusaidia kuingia na kusikiliza Mungu. Kuchukua muda kuomba—mazungumzo hayo rahisi na Mungu—hapo ndipo mahali pa kuanzia. Muulize swali hili: Ni nini unataka kufanya ndani yangu na kupitia kwangu mwaka huu? Swali hili litakusaidia kugundua neno lililokusudiwa kuwa lako. Usichukue neno zuri; pokea neno la Mungu. Hatua ya 3 – Ishi Kwa Neno Lako (Tazama Nje) – Mara tu utakapogundua neno lililokusudiwa kuwa lako, ni wakati wa kuliishi. Neno lako litakuwa na athari katika kila maeneo ya maisha yako: kimwili, kiakili, kiroho, kihisia, kiuhusiano na hata kifedha. Weka neno lako moja mbele na katikati. Waambie washirika wako wa uwajibikaji na familia yako kuhusu neno lako la mwaka. Liandike katika shajara yako. Libandike kwenye jokofu lako. Zungumzia neno hilo pamoja na familia yako kwa meza ya chakula. Fanya lolote uwezalo kuliweka kama lengo na kuliweka kuwa safi. Tunaomba kuwa mwaka huu utakuwa mwaka wa mafanikio kwako, Bwana akuinue na atumie Neno lako Moja kumletea utukufu!





Nenda


1. Ni nini Mungu anakuambia sasa kuhusu mada ya Neno Lako Moja?


2. Jitolee uwe na muda wa uaminifu wa kuomba na kumuuliza Mungu azungumze nawe.


3. Pitia hatua hizo tatu na uache Mungu akuonyeshe neno lililokusudiwa kuwa lako.





Zoezi


Zaburi 27:4; Zaburi 84





Muda wa ziada


""Bwana, naomba mwaka wa mafanikio. Tumia mada ya Neno hili Moja kukuletea utukufu. Ninyooshe katika mchakato huu wote. Nionyeshe ukweli na ufunuo. Tafadhali fanya yawe wazi kwangu. Ongea , Bwana, mtumushi Wako anasikiliza. Katika jina la Yesu, Amina."


siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

One Word That Will Change Your Life

NENO MOJA husaidia kurahisisha maisha yako kwa kulenga tu NENO MOJA kwa mwaka mzima. Urahisishaji wa kugundua neno ambalo Mungu amekuwekea inafanya kuwa kichochezi cha maisha yako kubadilika. Vurugu na utata husababisha ...

More

Tungependa kushukuru Jon Gordon, Dan Britton na Jimmy Page kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.getoneword.com

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha