Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Neno Moja Litakalobadilisha Maisha YakoMfano

One Word That Will Change Your Life

SIKU 2 YA 4

Neno Moja Tu





Weka


Ni vugumu kurahisisha maisha. Kufupisha lengo inaonekana haiwezekani. Mwaka uliopita, huenda uliulizwa mara kadhaa, "Unaendeleaje?" Jibu lako labda lilikuwa kitu kama, "Nimekuwa na shughuli nyingi sana!" hutasikia kamwe mtu yeyote akisema, "Nimekuwa na muda mwingi sana na ninatafuta kitu kipya cha kufanya." Mtu huyo hayupo.





Uko na mengi ya kufanya, na ratiba yako ni haina mwisho. Unajihisi kama unakimbia maishani. Ndio maana tunahitaji kuwa na kusudi la kufafanua na kurahisisha maisha. Tumekuwa tukijadili na watu wengi somo rahisi la kuunda neno moja tu kama mada ya mwaka ujao. Tuliamua kuacha kuorodhesha maazimio na kuanza kuishi Neno Moja. Ingawaje Biblia haina msemo ""Mada ya Neno Moja,""inavutia kujua kuwa msemo ""Kitu kimoja"" unaonekana mara tano katika Biblia: mara moja katika Wafilipi na mara nne katika Injili.





Katika Wafilipi 3:13-14, Paulo anatumia msemo ""kitu kimoja"" kuleta lengo na uwazi kwa wito wake. Katika Luka 10:42, Yesu anaambia Martha, ""Kitu kimoja tu kinahitajika."" Luka 18:22 na Marko 10:21 wanajumuisha maneno yake kwa tajiri na kudhihirisha ukosefu ya ""kitu kimoja."" Yohana 9:25 inajumuisha pia msemo huu wakati kipofu anapowaambia mafarisayo, ""Kitu kimoja najua. Nilikuwa kipofu lakini sasa naona!"" Kwa njia sawa ambayo maandiko yanatumia maneno haya, tunaweza pia kuyatumia kwa kumuuliza Mungu atuonyeshe mada ya Neno Moja kwetu mwakani.





Tulipoanza mchakato huu mara ya kwanza, nusu ya furaha ilikuwa kuchagua neno la mwaka, lakini tumejifunza kuwa sio lazima iwe ni sisi tunaochagua neno, lakini badala yake Mungu anatuonyesha. Mungu anaweza kwa ukweli angusha neno lililopakwa mafuta, neno maalum katika nafsi yako. Katika miaka yetu ya kwanza michache, tunakubali kuwa ilikuwa sisi tuliokuwa tukichagua neno na wachache sana wakipokea neno kutoka kwa Mungu.





Hata hivyo, Mungu bado aliyatumia! Lakini tulipopata uzoefu zaidi katika mchakato, tulijifundisha kisikiliza na kutazama Mungu akiongoza katika kuchagua neno. Kwa kusikiliza sauti ya Mungu, utagundua Neno kutoka kwa Mungu, sio tu neno nzuri.





Furahia mchakato na ukumbuke: Neno Moja Tu. SIo msemo. Sio hata maneno mawili. Fupisha lengo kwa ajili ya kubadilisha maisha. Neno Moja Tu!





Nenda


1. Kwa nini ni vigumu kurahisisha maisha? Kwa nini maisha haya ni magumu?


2. Kwa nini unafikiri huwa tunajaribu kuwafurahisha watu kwa mengi na wala sio machache?


3. Ni nini Mungu anakuambia sasa kuhusu mada ya Neno lako Moja la Mwaka? Jitolee uwe na muda wa maombi na kumuuliza Mungu kuongea nawe.








Zoezi


Luka 10:42; Luka 18:22; Marko 10:21





Muda wa Ziada


""Mungu Baba wa Mbinguni, ninaomba Neno Moja tu. Nataka neno moja kutoka kwako. Tafadhali nionekanie. Niko tayari kupokea neno ulilounda kwa ajili yangu. Katika jina la Yesu, Amina.""


siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

One Word That Will Change Your Life

NENO MOJA husaidia kurahisisha maisha yako kwa kulenga tu NENO MOJA kwa mwaka mzima. Urahisishaji wa kugundua neno ambalo Mungu amekuwekea inafanya kuwa kichochezi cha maisha yako kubadilika. Vurugu na utata husababisha ...

More

Tungependa kushukuru Jon Gordon, Dan Britton na Jimmy Page kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.getoneword.com

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha