Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Mambo yote ni mapyaMfano

All Things New

SIKU 2 YA 5

Kuna wakati nilifikiria kwamba kama nampenda mungu na kufanya uamuzi thabiti, wa kibiblia, nitabarikiwa na mtindo fulani wa maisha mazuri, yasiyo na kuvunjika moyo, au majnga, au magonjwa. Nilipoendelea kukua, nilianza kugundua kuwa kumwamini Mungu hakukuhakikishii maisha hayo bora na usalama. Bado, nilifikiria kwamba nilifanya sehemu yangu basi na Mungu na yeye atalazimika kufanya sehemu yake: kunijengea aina ya maisha tunayotamani Marekani na kunilinda na maumivu.


Kwa kumbu kumbu, ninaamini utii huzaa baraka na Mungu anapendezwa na kutupa zawadi za vitu na uhusiano, mara nyingi ikiwa ni kwa kumfuata yeye. Lakini bado, uelewa wangu wa jinsi mateso yanavyoingia--au kutokuingia==katika dhana kubwa ya maisha ya mkristo ulikuwa pungufu. Biblia inatuambia kwamba mateso yanaa sehemu yake katika maisha yetu, hata Waebrania 2:10 inaeleza kwamba Yesu alikamilishwa katika mateso. Kitu nilichokisahau katika kueleza kilichonifurahisha na kujaribu kujikinga na nilichokuwa nakiogopa " kuja kwaangu" (kwa maneno mengine ya Ayubu) ilikuwa kitu rahisi: mateso ni sehemu ya baraka.


Mawazo ya mateso tasituletee msumari wa hofu katika mioyo yetu kwa sababu Mungu yupo katika mateso yetu. Lakini hatupaswi kuendea maisha ya mateso, kufa, na kuathirika katika jina la Yesu. Kimsingi, tusiogope mateso, lakini hatutakiwi kuwa tunayatafuta pia.


Paulo anafungua waraka wake kwa Wakorintho kwa kukubali tabia mbili za Mungu kwamba hukutana nasi katika mateso. Angalia Paulo hakusema Mungu ni Baba mwenye rehema, japokuwa yuko hivyo, bali ni Baba wa rehema. Yeye ndiye mwanzo na asili ya huruma. Yeye ndiye chemchem ya kwanza na pekee ya huruma--Baba ambaye huruma zote zinatoka huko. Hii ni kuhamisha dhana kwa mtu ambaye anamuona Mungu kama mtu ambaye mara chache anaonesha upande wa mzuri tuu.


Hebu tuangalie upande wa asili ya lugha ya neno rehema (huruma). Lina maanisha “Matumbo ambako huruma hukaa, moyo wa huruma, hisia, shauku, kuonesha huruma" au " sehemu ya ndani." Tunapoangalia ufafanuzi wa neno hili, tunapata hisia kali sana. Kulingana na maandiko, nataka usikie leo kwamba Bwana anahisia nawe. Kwa huruma na rehema anakupenda.


siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

All Things New

Katika safari hii kwenye kitabu cha Wakorintho wa pili, mambo yote mapya yanavumbua theologia ya Paulo katika safari ya imani katika ulimwengu huu na wito wa Mungu kwetu kuwa jasiri. Kelly Minter anatusaidia kuelewa jins...

More

Tunapenda kuwashukuru LifeWay Women kwa kutoa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea: http://www.lifeway.com/allthingsnew

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha