Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Mambo yote ni mapyaMfano

All Things New

SIKU 1 YA 5

Maisha ya mkristo hakika ni kitendawili. Kile ambacho Yesu anakiona cha thamani ni tofauti na kile ambacho sisi katika hali ya kawaida tunakishikilia.


2 Wakorintho ni waraka wa tofauti. Ni waraka wa imani ya hatari wa kuweka tumaini letu lote kwa Mungu, hata kama tunatumainia nguvu zetu na fahari ya kutupeleka ambayo mara zote inaonekana salama na ya kueleweka. Ni kuhusu amani idumuyo ya kilindi cha nafsi zetu wakati dhambi zetu zinapokuwa hazihesabiwi hatia kwa sababu Mungu alimtuma mwanawe Yesu ulimwenguni, ambaye alizichukua dhambi zetu. Paulo anaita huu ni upatanisho.


Wakati Paulo alipowasili mwanzoni mwa 50 A.D., Korintho ilikuwa katika kilele cha maendeleo. Kitovu cha biashara cha Uyunani ya kusini, Korintho ilikuwa inastawi, tajiri, na imejaa mchanganyiko wa tamaduni za Kirumi na Kiyunani. Mji mkongwe wa Korintho ulikuwa na fahari ya kila kitu ambacho ungekitaka. Lakini kama tunavyojua: Kuweza kupata kila kitu tunachokitaka hakuishii siku zote kuwa vile tulivyofikiria tunataka. 


Utajiri wa utamaduni wa Korintho ulikuwa na mapungufu yake, kama ilivyo kwa majiji yetu ya sasa. Uasherati, utumwa, na tamaa za mwili za kila aina zilikuwepo katika mipaka yake. Miungu wa uongo ilikuwepo kila mahali.


Naona waraka huu ni wa kutia moyo sana kwa sababu kama kanisa lilifanya kazi Korintho, unaweza kufanya kazi hata katika maeneo ambayo wewe na mimi tunaishi. Nakubali kwamba wakati mwingine nadhani ulimwengu umeendelea sana na dhuluma, ubaguzi wa rangi, na ukiukwaji wa maadili. Hata hivyo, kama injili ya Yesu iliwabadilisha makahaba wa Korintho, matajiri, wapagani, na viongozi wa masinagogi, basi habari njema za Yesu Kristo zinaweza kuwabadilisha watu wa majiji yetu hata leo. Na ijapokuwa najaribiwa wakati fulani kufikiria kwamba watu wa Mungu wanapatikana katika mazingira ya dini, Mungu alikuwa na watu wake Korintho. Kama alivyo na wewe na mimi katika utamaduni tunaoishi. 2 Wakorintho inatukumbusha kwamba kanisa la Mungu linang'aa zaidi gizani kuliko mahali ambapo tayari kuna mwanga.


Unapopitia katika 2 Wakorintho, kuwa makini kuangalia vitu tofauti. Angalia jinsi Paulo anavyowapenda Wakorintho. Unapofikiria tofauti hizo za wazi wazi, usisahau kwamba umepewa uwezo wa kuishi vizuri na kutengwa kwa sababu--tangu mauti ya Yesu na ufufuko wake --utu wa kale umeondoka, na utu upya umekuja. Mara ya mwisho nimeangalia, uzamani na upya kuna tofauti.


siku 2

Kuhusu Mpango huu

All Things New

Katika safari hii kwenye kitabu cha Wakorintho wa pili, mambo yote mapya yanavumbua theologia ya Paulo katika safari ya imani katika ulimwengu huu na wito wa Mungu kwetu kuwa jasiri. Kelly Minter anatusaidia kuelewa jins...

More

Tunapenda kuwashukuru LifeWay Women kwa kutoa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea: http://www.lifeway.com/allthingsnew

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha