Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Siku Sita Za Majina Ya MunguMfano

Siku Sita Za Majina Ya Mungu

SIKU 6 YA 6

SIKU YA 6: EL SIMCHATH GILI – MUNGU FURAHA YANGU IPITAYO KIFANI

Fikiria kuhusu furaha unayopata unapokuwa stadi wa jambo fulani kwa mara ya kwanza. Labda ulijifunza lugha ya kigeni vizuri vya kutosha na hatimaye kuweza kuwasiliana na wazungumzaji asilia katika nchi nyingine. Au uliweka maili baada ya maili na hatimaye ukavuka mstari wa kumalizia wa mbio za marathoni. Labda umekuwa ukijaribu kwa miaka kupata digrii yako ya chuo kikuu, na hatimaye unapanda kwenye jukwaa hiyo ili kuchukua shahada yako. Unahisi hisia nyingi, lakini furaha iko mbele kila wakati.

Vitu vyote vyema hutoka kwa Mwenyezi Mungu, naye hufurahia kila jambo njema. Yeye ndiye chanzo pekee na cha kweli cha furaha, na tunapoweka tumaini letu kwake, tunaweza kupata furaha katika hali zetu zote. Tunaweza kuwa na furaha katikati ya mapambano, ikiwa tumaini letu liko kwa Bwana.

Makosa tunayofanya mara nyingi ni kutafuta furaha nje ya Mungu. Tunapojithamini kulingana na maoni ya mtu mwingine kutuhusu au mshahara tunaopata au nafasi yetu ya kijamii, tunakosa furaha ya kweli. Tunakosa furaha katika safari, furaha ya kugundua lolote lile, furaha ya moyo ulio wazi kwa Mungu.

Na pia tunakosa nafasi ya ajabu ya kushiriki furaha ya Bwana na wengine. Lakini tunapojazwa na furaha inayotoka kwa Mungu, upendo wake unaangaza toka ndani mwetu na raha kwa wale wanaotuzunguka na pia kujua furaha ya kweli.

Tunatumai kuwa mpango huu umekuhimiza. Ili ujue zaid kuhusu huduma ya Tony Evans, bofya hapa.

siku 5

Kuhusu Mpango huu

Siku Sita Za Majina Ya Mungu

Kutoka kwa majina mengi aliyo nayo Mungu, Yeye ametufunulia vipengele vya tabia yake na asili yake. Zaidi ya majina haya ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, Biblia inaonyesha majina zaidi ya 80 tofauti ya Mungu. Hapa kuna...

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha