Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Siku Sita Za Majina Ya MunguMfano

Siku Sita Za Majina Ya Mungu

SIKU 4 YA 6

SIKU YA 4: ESH OKLAH – MOTO ULAO

Je, umewahi kushuhudia uharibifu uliosababishwa na moto wa msitu? Inakula kila kitu katika njia yake, kuruka haraka juu ya barabara na madaraja na hata mito. Sasa fikiria moto unaoteketeza ambao ni mkubwa kuliko ulimwengu, nawe utaanza kupata mtazamo mdogo wa nguvu za Mungu.

Tunapaswa kuheshimu nguvu nyingi sana za Mungu, lakini pia tunapaswa kukumbuka kwamba Yeye ni Mungu wa kibinafsi sana ambaye anatujali sana. Na kwa sababu hii, yeye ni Mungu ambaye anastahili sifa na ibada zetu nyakati zote. Hatupaswi kumchukulia kirahisi, lakini pia tusiogope kumlilia na kuingia katika uhusiano naye.

Kufahamu ukuu wa Mungu kunaweza kuwa ni jambo ngumu, vile vile yaweza kuwa kuhusu umaakini wake kwa kila maelezo ya maisha yetu. Je, huyu Mkuu na Mwenye Nguvu sana anawezaje kuwa na shughuli sana na mambo yanayoonekana kuwa madogo ya maisha yetu? Ni kwa sababu anatujali sana. Na ndio maana tunahitaji kuruhusu moto wake ulao uwake kwa nguvu mioyoni mwetu.

Yeye ni Esh Oklah, moto ulao, lakini moto uliojaa neema na subira na huruma. Anatuvuta kwake kwa lengo la sisi kumfanya yeye kuwa wa kwanza katika mioyo, akili na roho zetu. Na katikati ya moto, Yeye hupanda upendo katika mioyo yetu.

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Siku Sita Za Majina Ya Mungu

Kutoka kwa majina mengi aliyo nayo Mungu, Yeye ametufunulia vipengele vya tabia yake na asili yake. Zaidi ya majina haya ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, Biblia inaonyesha majina zaidi ya 80 tofauti ya Mungu. Hapa kuna...

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha