Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Ndoa Ya UfalmeMfano

Ndoa Ya Ufalme

SIKU 2 YA 5

Neno ndoa ya ufalme linasadikisha kuwa kuna ufalme. Ikiwa kuna ufalme, basi dhana ni kwamba kuna mfalme. Ikiwa kuna mfalme, basi dhana ni kwamba kuna raia ambao mfalme anawatawala. Na hatimaye, ikiwa kuna raia katika ufalme, dhana ni kwamba kuna sheria ambazo wanapaswa kuishi nazo. Kwa hivyo, tunaposema ndoa ya ufalme, tunarejelea ndoa inayofanya kazi kulingana na ufalme. Ufalme maalum. Ufalme wa Mungu.

Katika Biblia nzima, ufalme wa Mungu unaashiria utawala au mamlaka Yake. Neno lingine ambalo maandiko yanatumia kuelezea utawala wake ni ukuu. Kwa urahisi, hii ina maana kwamba Mungu ndiye anayesimamia kila kitu kabisa, na ufalme Wake pia una madhumuni yanayojumuisha yote—kwa kila kitu na kila mtu kumletea utukufu. Kitovu cha mada ya Biblia na jambo kuu linaloliunganisha, ni utukufu wa Mungu unaoonyeshwa kupitia maendeleo ya ufalme wake. Na kwa kuwa ndoa iko chini ya ufalme wake, basi tunaweza kuhitimisha kuwa ipo pia ili kumletea utukufu.

Hata hivyo, wanadamu hupinga siku zote kumpa Mungu utukufu. Uumbaji unaonyesha utukufu wa Mungu kila siku, kama vile alivyouumba ufanye. Lakini wanadamu wanaonekana kujitakia utukufu. Tunataka kufanya mambo kwa njia yetu, si kwa njia ya Mungu. Waumini wengi wanatatizika katika ndoa zao kwa sababu wanataka Mungu atimize matamanio yao kupitia ndoa badala ya ndoa yao kumletea utukufu. Wanahangaikia zaidi furaha, urafiki, fedha, kutosheka kingono na wingi wa manufaa mengine ambayo ndoa huleta, huku wakisahau kusudi la kiungu lililowekwa. Kwa maneno mengine, wanamtaka Mungu abariki ajenda yao badala ya kutafuta kufuata ajenda yake.

Lakini hiyo sio ndoa ya kifalme. Mume na mke wanapoiga kielelezo cha ndoa ya ufalme kwa ulimwengu unaowatazama kwa jinsi wanavyojitiisha chini ya utawala wake, wanasaidia kuendeleza ufalme wa Mungu, naye hutukuzwa.

Je! ni kwa njia gani utamaduni wetu wa kisasa umeunda ndoa yako kuelekea ajenda ya kujitosheleza?

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Ndoa Ya Ufalme

Ndoa huja na furaha nyingi na changamoto kubwa. Sababu mojawapo ya changamoto hizo ni kwa sababu tumesahau kusudi la kibiblia la ndoa. Tumemuondoa Mungu na kufafanua ndoa kwa msingi ya furaha. Lakini ndoa ipo ili kumtuku...

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha