Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Ndoa Ya UfalmeMfano

Ndoa Ya Ufalme

SIKU 1 YA 5

Wanandoa wanapotangaza uchumba wao, watu wengi wanataka kusikia "hadithi yao." Walikutana vipi? Ilikuwa ni upendo walipo onana mara ya kwanza? Je! walikuwa wapenzi wa utotoni, au walikutana baadaye maishani? Vyo vyote itakavyokuwa, hadithi ya asili ya wanandoa hutuvutia.

Umewahi kufikiria kuhusu mwanzo wa hadithi ya ndoa yenyewe? Ikiwa unataka kuwa na ndoa yenye afya, jambo la kwanza unapaswa kuelewa ni kwamba ndoa ni wazo la Mungu. Na kwa sababu aliiumba, ni lazima tumwendee kwa ufafanuzi na ufahamu wake. Hii ina maana kwamba ndoa yako, bila kujali mwanzo wake, inapoletwa chini ya utawala wa Mungu, uhusiano wako unaweza kusitawi na kuwa vile Mungu alivyokusudia iwe.

Kutoka kwa Maandiko, tunagundua kwamba Mungu aliumba ndoa ili kupanua ufalme wake katika historia ya mwanadamu. Ndoa ya ufalme ni “muungano wa agano kati ya mwanamume na mwanamke wanaojitolea kufanya kazi kwa umoja chini ya mamlaka ya kimungu, kusudi ni watoe nakala ya mfano wa Mungu na kupanua utawala Wake ulimwenguni kupitia miito yao ya kibinafsi na ya pamoja.” Hayo ni maneno yajazayo kinywa, kwa hivyo unaweza taka kurejea kusoma tena. Lakini kwa ufupi, dhamira ya ndoa ni kurudufu sura ya Mungu katika historia na kutekeleza agizo lake la kuwaacha wanadamu watawale.

Kwa hivyo, ndoa sio tu mkataba wa kijamii. Wala furaha sio lengo lake. Hili ni mojawapo ya matatizo makuu ambayo ndoa nyingi hukabiliana nazo leo. Wanandoa huhusiana na ndoa tu kupitia masharti ya kijamii na kihisia. Ni lazima turudi kwenye ufahamu wa kibiblia wa ndoa. Mungu aliiumba kama agano takatifu, lenye jukumu la kuakisi sura yake na kuendeleza ufalme wake. Furaha ni faida ya ndoa, lakini sio lengo la ndoa. Lengo ni kuakisi Mungu kwa kuendeleza ufalme wake duniani. Furaha hutokea kama chipukizi asilia wakati lengo la kibiblia linafuatwa.

Jambo la msingi ni kwamba ndoa ni dhana ya ufalme, si ya kijamii tu.

Ni jinsi gani kufanya furaha kuwa lengo la ndoa kunaunda matatizo katika ndoa ya mtu?

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Ndoa Ya Ufalme

Ndoa huja na furaha nyingi na changamoto kubwa. Sababu mojawapo ya changamoto hizo ni kwa sababu tumesahau kusudi la kibiblia la ndoa. Tumemuondoa Mungu na kufafanua ndoa kwa msingi ya furaha. Lakini ndoa ipo ili kumtuku...

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha