Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Wema Wetu Na Utukufu WakeMfano

Wema Wetu Na Utukufu Wake

SIKU 2 YA 3

Lengo kuu la Mungu daima matokeo yake ni utukufu wa Mungu. Waefeso sura ya kwanza inakazia hili kwa ajili yetu

Katika pendo alituchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo sawasawa na Uradhi wa mapenzi yake. Na usifiwe utukufu wa neema yake …Nasi katika huyo tupate kuwa sifa ya utukufu wake, sisi tuliotangulia kumwekea Yesu tumaini letu …ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake. (Aya. 4b–6a, 12, 14b)

Sababu ya kimsingi ambayo Mungu anafanya kila jambo kwa matokeo yake yaliyokusudiwa ni “kwa sifa ya utukufu wake.” Mungu huweka dhamana ya kuhakikisha kwamba kila kitu alichoumba kinatimiza na kutosheleza kusudi lake lililokusudiwa, ambalo ni kumrudishia yeye utukufu.

Penda au usipende, Mungu yupo kwa ajili ya utukufu wake mwenyewe. Sasa, unaweza kuupiga vita ukweli huo, kugombana kuhusu, kuupinga, kutoutaka, kuukataa, kuushtaki ama jambo lingine lolote unalotaka kufanya. Lakini chochote unachofanya kuhusu hilo, hakitaweza kuubadilisha. Mungu yupo kwa ajili ya Mungu. Vivyo hivyo kila alichokifanya. Aliifanya yote kwa ajili yake. Hiyo ndiyo sababu iko hapa. Hiyo ndiyo sababu tuko hapa. Tumeumbwa kwa ajili ya Mungu. Maisha yetu si kwa ajili yetu sisi; yanamhusu yeye na utukufu wake. Ikiwa haujali sana kuhusu hilo, basi nenda na utengeneze ulimwengu wako mwenyewe. Alitengeneza hii, kwa hiyo anamamlaka ya kuweka masharti,

Chochote kinachoshindana na, kukataa au kudharau utukufu wa Mungu kipo katika hali ya kudumu ya kupotoshwa. Ni nje ya utaratibu. Mungu aliumba vitu vyote ili kuonyesha sifa, tabia na uwezo wake.

Hata hivyo, kuna sababu nyingine inayofanya Mungu afanye mambo yote yafanye kazi pamoja. Anafanya hivyo kwa utukufu wake, ndiyo, lakini pia anafanya kwa ajili yetu—kwa wema. Utakumbuka Warumi 8:28 inasema, “Mungu hufanya vitu vyote vifanye kazi pamoja kwa wema…” Kimsingi, hiyo ina maana kwamba analeta manufaa yetu. Neno wema linamaanisha “kile chenye manufaa.” Hivyo, Mungu pia anatafuta kuleta manufaa na baraka katika maisha ya wale wanaompenda na kutembea kulingana na njia za kusudi lake.

Tafadhali usisome vibaya aya hiyo na kuifanya itumike kwa kila mtu, kila mahali. Watu wengi sana hufanya hivyo. Haisemi kwamba Mungu husababisha vitu vyote kwa kila njia kufanya kazi kwa wema. La hasha! Inahusu haswa wale wanaompenda na walioitwa kulingana na kusudi lake. Kwa hivyo, kuna ubaya katika ulimwengu huu. Mambo yasiyotamanika hutendeka. Dhana ambayo mara nyingi huwepo yanapotendeka ni kwamba Mungu lazima asiwe mwema Mwenyewe. Lakini uwepo wa giza haukatazi nguvu ya nuru. Nuru ipo ili kuliondoa giza, na si kuliondoa kabisa.

Warumi 8:28 haisemi kwamba Mungu hufanya vitu vyote kuwa vyema. Badala yake, yeye huunganisha vitu vyote kufanya kazi pamoja kwa ajili ya wema katika maisha ya wale wanaompenda na kufuata njia zake. Mkono wake ni ule usioonekana unaofanya kazi nyuma ya pazia la wema, mbaya na baya maishani. Anatengeneza na kuendesha mazingira mengi kuelekea lengo lake alilokusudia.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Wema Wetu Na Utukufu Wake

Katika mpango huu kusoma kwa ufahamu, Mchungaji na mwandishi mashuhuri Tony Evans anaelezea jinsi kila kitu tunachofanya ni kulingana na kusudi kuu la Mungu, na yote hufanya kazi kulingana na mapenzi yake kwa wema wetu n...

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha