Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Wema Wetu Na Utukufu WakeMfano

Wema Wetu Na Utukufu Wake

SIKU 1 YA 3

Je, umewahi kufikiria kuhusu athari za udhibiti mkuu wa Mungu juu ya kila kitu? Ikiwa Mungu ndiye ameshikilia usukani wa kila kitu, basi kila kitu ambacho wewe na mimi tumepewa ni matokeo ya moja kwa moja ya Mungu kuamua kufanya hivyo. Hakuna kitu chochote ambacho umepokea kisicho umbwa na Mungu au kuumbwa kwa vitu ambavyo Mungu aliviumba.

Unaweza kutaka kusoma sentensi hiyo tena. Na labda urudie tena, kwa kipimo kizuri.

Ni muhimu

Mungu hutengeneza kila kitu. Kwa sababu anafanya hivyo, anadai udhibiti juu ya hayo yote pia. Yeye ndiye anadhibiti vyote. Yeye ndiye mkamlifu, mwenye uamuzi wa mwisho na meneja wa kila kitu katika kinaga naga. Anahusika katika kila kitu kutoka moyoni kwa utatanishi na undani sana. Anasimamia ulimwengu na sisi sote ndani yake kwa kiwango cha juu kabisa kiwezekanacho. Na kama hangefanya hivyo—kama angelichukua muda kidogo tu kurudi nyuma na kutoshikilia ulimwengu mahali pake—sisi sote tungeangamizwa mara moja.

Kutoka kwa nafasi yake nzuri ya mtazamo, yote yana maana kamili. Lakini kutoka kwa upande wetu, muda unaweza kuonekana kuwa na alama ya safu nyingi zisizo na mwisho au mfululizo wa dharura ambazo tunaweza kuziita "bahati," "kiajali" au hata "matukio ya kiholela"

Lakini ndivyo inavyoonekana; ila si ndivyo jinsi ipo.

Kwa sababu hakuna jambo la kiholela kwa Mungu. Anafanyia kazi bayana kila ncha, sio tu kutazama kikitokea. Kilicho zaidi ni kwamba anafanyia kazi kila kitu kuelekea lengo lake alilokusudia. Mara wewe na mimi tunapofikia kiwango cha kuelewa lengo lake kuu, tunaweza kuanza kuelewa njia zake.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Wema Wetu Na Utukufu Wake

Katika mpango huu kusoma kwa ufahamu, Mchungaji na mwandishi mashuhuri Tony Evans anaelezea jinsi kila kitu tunachofanya ni kulingana na kusudi kuu la Mungu, na yote hufanya kazi kulingana na mapenzi yake kwa wema wetu n...

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha