Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 2 - Matendo ya MitumeMfano

BibleProject | Ufalme Unaoenda  Kinyume na Matarijio  / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume

SIKU 2 YA 20

Baada ya Yesu kupewa ufalme mbinguni, Luka anatuambia kuwa wanafunzi wako pamoja katika siku ya Pentekoste. Hii ni sikukuu ya kale ya Waisraeli ya kila mwaka, ambapo maelfu ya mahujaji wa Kiyahudi walisafiri hadi Yerusalemu ili kusherehekea. Wakati wa tukio hilo, wanafunzi wa Yesu walikuwa wakiomba, kisha ghafla sauti ya upepo mkali ilijaza chumba na waliona ndimi za moto zikiwa juu ya kichwa cha kila mmoja wao. Je, taswira hii ya ajabu inahusu nini?

Hapa, Luka anaangazia dhamira iliyorudiwa ya Agano la Kale ambapo uwepo wa Mungu unaonekana kama moto pia. Kwa mfano, Mungu alipofanya agano na Israeli katika Mlima wa Sinai, uwepo wake ulionekana kama ndimi za moto kileleni mwa mlima (Kutoka 19:17-18). Uwepo wa Mungu ulijitokeza pia kama nguzo ya moto alipojaza hema ili kukaa miongoni mwa Israeli (Hesabu 9:15). Hivyo Luka anapofafanua kuhusu moto kuwatembelea watu wa Mungu, tunafaa kutambua hiyo historia. Ila tu wakati huu, moto unatawanyika kuwa ndimi nyingi za moto juu ya watu wengi, badala ya kuonekana katika nguzo moja juu ya mlima au jengo. Hili linawasilisha jambo la kushangaza. Wanafunzi wanakuwa hekalu jipya linalotoka katika eneo moja hadi lingine ambako Mungu anaweza kukaa na kushiriki habari zake njema.

Uwepo wa Mungu haujazuiwa tena katika eneo moja. Sasa unaweza kuishi ndani ya binadamu wanaomtegemea Yesu. Luka anatuambia kuwa punde tu wafuasi wa Yesu walipopokea moto wa Mungu, walianza kuongea habari njema kuhusu Ufalme wa Yesu katika lugha ambazo hawakuzifahamu hapo awali. Mahujaji wa Kiyahudi wanashangaa kuwa wanaweza kuwaelewa vikamilifu. Bado Mungu hajakata tamaa kuhusu mpango wake wa kushirikiana na Israeli ili kubariki mataifa yote. Na katika wakati unaofaa tu, katika Pentekoste, siku ambayo wawakilishi kutoka makabila yote ya Israeli wanarejea Yerusalemu, anamtuma Roho wake kutangaza habari njema za Mfalme wa Israeli, Yesu ailiyesulubiwa na kufufuka. Maelfu walisikia ujumbe huu kwa lugha zao asili na wakaanza kumfuata Yesu siku hiyo hiyo.

Soma, tafakari, kisha Ujibu:

• Ulivysoma Matendo ya Mitume 2, ni maneno yapi au virai (vifungu vya maneno) viliteka umakinifu wako zaidi?

• Kumbuka maneno ya Yohana Mbatizaji tena (tazama Luka 3:16-18) na kumbuka kwamba waandishi wa biblia mara nyingi hutumia makapi kama mfano ya dhambi. Tafakari kuhusu kusudi la utakaso wa moto wakati wanafunzi wanavyopokea Roho wa Mungu. Unatambua nini?

• Linganisha moto wa Mungu katika Kutoka 19:17-18, Hesabu 9:15, na Matendo ya Mitume 2:1-4. Unatambua nini?

• Linganisha Yoeli 2:28-29 na Matendo ya Mitume 2:38-39 na tambua jinsi neno “wote” limetumika katika vifungu hivi. Hakuna aliyetengwa katika mwaliko, lakini “wote” wanaupokea vipi?

• Geuza kusoma kwako na tafakari yako kuwa ombi. Ongea na Mungu kuhusu maelezo yoyote katikakusoma kwako yaliyokushangaza, na uombe Roho wake Mtakatifu akusaidie kuelewa ukweli kuhusu Yesu na Ufalme wake.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Ufalme Unaoenda  Kinyume na Matarijio  / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume

BibleProject ilibuni Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarajio Sehemu ya 2 ili kuwatia watu moyo, vikundi vidogo, na familia mbali mbali waweze kusoma Matendo ya Mitume kwa siku 20. Mpango huu unajumuisha video za katuni, mih...

More

Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha