Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 2 - Matendo ya MitumeMfano

BibleProject | Ufalme Unaoenda  Kinyume na Matarijio  / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume

SIKU 4 YA 20

Tunapoendelea kusoma, tunaona vuguvugu la Yesu likiendelea kuongezeka kwa kasi, Wayahudi kutoka mataifa mengine wanapoanza kumfuata Yesu. Wanapopokea uwezo wa Roho Mtakatifu, maisha yao yanabadilika, na jamii inaanza kuishi kwa njia mpya kabisa, ikiwa imejawa furaha na ukarimu. Wanakula vyakula vya kila siku pamoja, wanaomba pamoja mara kwa mara, na hata wanauza vitu vyao ili kuwasaidia maskini walio miongoni mwao. Wanajifunza maana ya kuishi chini ya agano jipya, ambapo uwepo wa Mungu unaishi ndani ya watu badala ya hekalu.

Huenda unajua kuhusu simulizi ya ajabu katika kitabu cha Walawi inayohusu makuhani wawili waliomkosea Mungu heshima katika hekalu na kisha wakafa ghafla. Katika somo lililoteuliwa la leo, Luka anasimulia simulizi inayofanana na hiyo kuhusu watu wawili walioleta fedheha katika hekalu jipya la Roho Mtakatifu na kufa. Wanafunzi wanatiwa hofu. Wanaelewa uzito wa hili agano jipya na kupokea onyo, na uovu katika hekalu jipya unaondolewa. Lakini uovu katika jengo la hekalu la zamani unaendelea, viongozi wa dini wa hekalu wanaendelea kupambana dhidi ya wafuasi wa Yesu na ujumbe wake. Kuhani mkuu na maafisa wake wanatishiwa sana na mitume hadi wanawafunga gerezani tena, lakini malaika anawaondoa kwenye gereza na kuwaambia waende hekaluni ili kuendelea kuhubiri ujumbe wa Ufalme wa Yesu. Viongozi wa dini wanasisitiza kuwa mitume waache kumhubiri Yesu lakini mitume wanaendelea. Kufikia hapa, viongozi wa dini wako tayari kuwaua mitume, lakini kiongozi anayeitwa Gamalieli anawazuia kwa kusema, ikiwa ujumbe wao unatoka kwa Mungu, hakuna chochote kitakachoweza kuuangusha.

Soma, Tafakari, kisha Ujibu:

• Unafikiri Anania na Safira walifikiri wangepoteza nini ikiwa wangesema ukweli kuhusu mchango wao? Walichagua kufanya nini ili kujikinga dhidi ya hasara hiyo, na ni nini kilifanyika baadaye (tazama 5:1-11)?

• Unafikiri mitume walifikiri wangepoteza nini ikiwa wangemtii Mungu badala ya viongozi wa dini? Walichagua kufanya nini licha ya kile ambacho wangepoteza, na ni nini kilifanyika baadaye (tazama 5:29 na 5:40)? Wanafunzi walihisi vipi kuhusu matokeo ya kutii kwao (tazama 5:41-42)?

• Tafakari maneno yenye umri wa miaka 2000 ya Gamalieli (5:34-39) na ukweli kuwa ujumbe wa Yesu unaendelea kubadilisha ulimwengu leo. Hili linaleta mawazo, maswali au hisia zipi kwako?

•Ruhusu kusoma kwako na tafakari yako kuwa maombi kutoka moyoni mwako. Dhihirisha shukrani zako kwa ujumbe usioweza kusimamishwa wa Mungu. Kuwa mkweli kwake kuhusu kila kitu na uombe Roho wake akujaze na ujasiri na kuamini unakohitaji ili umtii licha ya gharama yake.

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Ufalme Unaoenda  Kinyume na Matarijio  / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume

BibleProject ilibuni Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarajio Sehemu ya 2 ili kuwatia watu moyo, vikundi vidogo, na familia mbali mbali waweze kusoma Matendo ya Mitume kwa siku 20. Mpango huu unajumuisha video za katuni, mih...

More

Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha