Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022

SIKU 4 YA 28

Paulo anatoa sala ya shukrani. Anamshukuru Mungu kwa yale anayoyafanya kwa maisha ya Wakristo wa Efeso (m.15-16,Kwa sababu hiyo mimi nami, tangu nilipopata habari za imani yenu katika Bwana Yesu, na pendo lenu kwa watakatifu wote, siachi kutoa shukrani kwa ajili yenu; nikiwakumbuka katika sala zangu), na anaomba kwamba baraka zilizofafanuliwa katika m.3-14 ambazo Mungu amezitoa, zitatimia kikamilifu katika maisha yao (ukirudia m.17-23, tafuta kuziorodhesha baraka hizo). Hasa Paulo anaomba kuwa watakuwa na uelewa wa kina kuhusu mpango wa Mungu wa wokovu na nafasi yao katika mpango huo. Inawezekana Mungu amefanya mengi katika maisha yako na ya waumini wenzako. Je, wewe huwa unamshukuru Mungu kwa hayo yote na kuwaombea?

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022

Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu uliloso...

More

Tungependa kushukuru Soma Bible kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha