Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 07/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

SIKU 6 YA 31

Mfano wa leo unahusu juya au nyavu iliyotupwa baharini. Pamoja na mfano ule wa mbegu njema na magugu, mfano huu unasisitiza mambo mawili muhimu:1.Husisitiza kwamba iko siku ambapo wanadamu wote watafika mbele ya Mwana wa Mungu, walio hai na wafu (m.40-41, Kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni, ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia.Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi; m.49, Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki). Na kwa Yesu hakuna upendeleo. Atahukumu kwa haki kabisa, wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu(Ebr 4:13). 2.Yesu anasisitiza kwamba uzima wa milele upo ambapo wenye haki watang'aa kama jua katika ufalme wa Baba yao(m.43), na pia moto wa milele upo. Watendao maasi watatupwa katika tanuru ya moto(m.42), maana malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki, na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno(m.49-50). Yesu anatuambia ukweli mtupu ili kutuonya, maana hapendi tupotee. Je, unaelekea wapi?

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

Soma Biblia Kila Siku 07/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kuji...

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha