Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 07/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

SIKU 8 YA 31

Naye Yesu aliposikia hayo, aliondoka huko katika chombo, akaenda mahali pasipo watu, faraghani(m.13). Yesu alikuwa amesikia nini? Jibu linapatikana katika m.1-2 na Lk 13:31: Wakati ule mfalme Herode alisikia habari za Yesu, akawaambia watumishi wake,Huyo ndiye Yohana Mbatizaji; amefufuka katika wafu; na kwa hiyo nguvu hizo zinatenda kazi ndani yake. … Saa ile ile Mafarisayo kadha wa kadha walimwendea, wakamwambia, Toka hapa, uende mahali pengine, kwa sababu Herode anataka kukuua. Maisha ya Yesu yalikuwa hatarini, lakini wakati wake ulikuwa bado haujatimia. Kwa hiyo aliepukana na hiyo hatari kwa kufanya mambo mawili, na katika hili ni mfano kwetu. 1.Alitumia akili yake: aliondoka huko. Aliamua kwenda kwenye eneo la mfalme mwingine (Lk 9:10, Yesu akawachukua [wanafunzi wake], akaenda nao faraghani mpaka mji mmoja uitwao Bethsaida). 2.Alimkimbilia Baba yake katika sala: akaenda ... faraghani.

siku 7siku 9

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

Soma Biblia Kila Siku 07/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kuji...

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha