Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kusikia Kutoka Kwa Mungu Kila AsubuhiMfano

Kusikia Kutoka Kwa Mungu  Kila Asubuhi

SIKU 3 YA 14

Kimbilio La Kwanza


Ee Mungu, Mungu wangu nitakutafuta mapema… (ZABURI 63:1)


Wakati mwingine huwa nashangazwa na jinsi tunavyochukua muda mrefu tuking’ang’ana katika hali kabla ya kuongea na Mungu kuhusu hali hiyo na kusikiliza sauti yake. Tunalalamika kuhusu shida zetu; tunanung’unika; tunanong’ona; tunawaambia marafiki zetu jinsi ambavyo tungependa Mungu afanye kitu kuhusu hali hiyo. Tunang’ang’ana na hali katika mawazo yetu na hisia zetu, huku tukikosa kutumia suluhu rahisi tuliyo nayo: sala. Pengine hata jambo baya kuliko hilo ni kwamba tunatoa taarifa ya kushangaza inayojulikana na binadamu kama: “Sina lingine la kufanya ila kuomba”. Nina hakika umesikia matamshi kama hayo awali na labda hata umewahi kusema hivyo. Sisi wote tumewahi. Sisi wote tuna hatia ya kufanya sala kuwa suluhu ya mwisho katika jitihada zetu na kusema mambo kama vile, “Sasa, hakuna lingine linalofanya kazi, pengine sasa inafaa tuombe.” Wajua hilo linaniambia nini? Linaniambia kwamba hatuamini katika nguvu za sala jinsi inavyostahili. Tunabeba mizigo tusiyofaa kubeba- na maisha ni magumu kuliko yalivyo- kwa sababu hatutambui jinsi sala zilivyo na nguvu. Iwapo tungejua, tungezungumza na Mungu na kusikiza anachosema kuhusu kila kitu, sio kama suluhu ya mwisho, lakini kama kimbilio la kwanza.


NENO LA MUNGU KWAKO LEO


Acha sala ziwe kimbilio lako la kwanza wala si kama suluhu ya mwisho.

Andiko

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Kusikia Kutoka Kwa Mungu  Kila Asubuhi

Ibada hii inatoa mawaidha mafupi, yenye kuwezesha ambayo yatakuhimiza na kukusaidia kupanga wakati na Mungu kipaumbele chako cha juu, kukuza hamu ya muda wa kila siku naye, kuelewa majibu yake kwa maombi yako, na kudumis...

More

Tunapenda kuwashukuru Joyce Meyer Mawaziri kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tv.joycemeyer.org/kiswahili/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha