Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA SABAMfano

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA SABA

SIKU 3 YA 7

  

KIFO CHA YOHANA MBATIZAJI

1 Wakati huo, Mfalme Herode aliyekuwa mtawala alisikia habari kuhusu sifa za Yesu, akawaambia watumishi wake,

“Huyu ni Yohana Mbatizaji, amefufuka kutoka kwa wafu! Hiyo ndiyo sababu nguvu za kutenda miujiza zinafanya kazi ndani yake.”

3 Herode alikuwa amemkamata Yohana akamfunga na kumweka gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, ndugu yake,

4 kwa kuwa Yohana alikuwa amemwambia Herode kwamba, “Si halali kwako kuwa na huyo mwanamke.”

5 Herode alitaka sana kumwua Yohana, lakini akaogopa watu kwa maana walimtambua kuwa ni nabii.

6 Katika siku ya kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa kwa Herode, binti wa Herodia alicheza mbele ya watu waliohudhuria akamfurahisha sana Herode

7 kiasi kwamba aliahidi kwa kiapo kumpa huyo binti lo lote atakaloomba.

8 Yeye akiwa amefundishwa na mama yake, huyo binti akasema, “Nipatie kichwa cha Yohana Mbatizaji kwenye sinia.”

9 Mfalme akasikitika, lakini kwa ajili ya kile kiapo alichoapa mbele ya wageni, akaamuru kwamba apatiwe ombi lake.

10 Hivyo akaagiza Yohana Mbatizaji akatwe kichwa mle gerezani.

11 Kichwa chake kikaletwa kwenye sinia, akapewa yule binti, naye akampelekea mama yake.

12 Wanafunzi wa Yohana wakaja na kuuchukua mwili wake kwenda kuuzika.

Kisha wakaenda wakamwambia Yesu.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA SABA

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadi...

More

Tunapenda kushukuru GNPI Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha