Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA SABAMfano

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA SABA

SIKU 1 YA 7

  

MFANO WA MAGUGU, PUNJE YA HARADALI, CHACHU

24 Yesu akawaambia mfano mwingine, akasema:

“Ufalme wa Mbinguni unaweza kufananishwa na mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake.

25 Lakini wakati kila mtu alipokuwa amelala, adui yake akaja na kupanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.

26 Ngano ilipoota na kutoa masuke, magugu nayo yakatokea.

27 “Watumishi wa yule mwenye shamba wakamjia na kumwambia, ‘Bwana, si tulipanda mbegu nzuri shambani mwako? Basi, magugu yametoka wapi?’

28 “Akawajibu, ‘Adui ndiye aliyefanya jambo hili.’“Wale watumishi wakamwuliza, ‘Je, unataka twende tukayang'oe?’

29 “Lakini akasema, ‘Hapana, msiyang'oe, kwa maana wakati mking'oa magugu mnaweza mkang'oa na ngano pamoja nayo.

30 Acheni ngano na magugu vikue vyote pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati huo nitawaambia wavunaji, wayakusanye magugu kwanza, wayafunge matita matita ili yachomwe moto, kisha wakusanye ngano na kuileta ghalani mwangu.’ ”

31 Akawaambia mfano mwingine, akasema,

“Ufalme wa Mbinguni ni kama punje ya haradali, ambayo mtu aliichukua akaipanda shambani mwake.

32 Ingawa mbegu hiyo ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini inapokua ni mmea mkubwa kuliko yote ya bustanini, nao huwa mti mkubwa, hata ndege wa angani huja na kutengeneza viota katika matawi yake.”

33 Akawaambia mfano mwingine,

“Ufalme wa Mbinguni unafanana na chachu ambayo mwanamke aliichukua akaichanganya katika vipimo vitatu vya unga mpaka wote ukaumuka.”

34 Yesu alinena mambo haya yote kwa makutano kwa mifano. Wala pasipo mfano hakuwaambia lo lote.

35 Hii ilikuwa ili kutimiza lile lililonenwa kwa vinywa vya manabii kusema:“Nitakifungua kinywa changu niseme nao kwa mifano,nitahubiri mambo yaliyofichika tangu kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu.”

36 Kisha Yesu akaagana na makutano, akaingia nyumbani. Wanafunzi wake wakamjia wakamwambia,

“Tueleze maana ya ule mfano wa magugu shambani.”

37 Akawaambia, “Aliyepanda mbegu nzuri ni Mwana wa Adamu.

38 Shamba ni ulimwengu na mbegu nzuri ni wana wa Ufalme. Magugu ni wana wa yule mwovu.

39 Yule adui aliyepanda magugu ni ibilisi. Mavuno ni mwisho wa dunia, nao wavunaji ni malaika.

40 “Kama vile magugu yang'olewavyo na kuchomwa motoni, ndivyo itakavyokuwa wakati wa mwisho wa dunia.

41 Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika Ufalme wake kila kitu kinachosababisha dhambi na watenda maovu wote.

42 Nao watawatupa katika tanuru la moto ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.

43 Ndipo wenye haki watang'aa kama jua katika Ufalme wa Baba yao.

aliye na masikio, na asikie.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA SABA

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadi...

More

Tunapenda kushukuru GNPI Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha