Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA MBILIMfano

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA MBILI

SIKU 3 YA 7

  

KUJARIBIWA KWA YESU

MATTHEW 27

Wale waliokuwa wamemkamata Yesu wakampeleka kwa Kayafa, Kuhani Mkuu, mahali ambapo walimu wa sheria pamoja na wazee walikuwa wamekusanyika.

Lakini Petro akamfuata kwa mbali mpaka uani kwa Kuhani Mkuu. 

Akaingia ndani akaketi pamoja na walinzi ili aone litakalotukia.

Basi viongozi wa wazee, makuhani na baraza lote wakatafuta ushahidi wa uongo dhidi ya Yesu ili wapate kumwua.

"Lakini hawakupata jambo lo lote, ingawa mashahidi wengi wa uongo walijitokeza.Hatimaye wakajitokeza mashahidi wawili wa uongo"

Hatimaye wakajitokeza mashahidi wawili wa uongo na kusema, 

“Huyu mtu alisema, ‘Ninaweza kulivunja Hekalu la Mungu na kulijenga tena kwa siku tatu.’ ”

Kisha Kuhani Mkuu akasimama na kumwambia Yesu,

“Je, wewe hutajibu? Ni ushahidi wa namna gani hawa watu wauletao dhidi yako?”

Lakini Yesu alikuwa kimya.Ndipo Kuhani Mkuu akamwambia, 

“Nakuapisha mbele za Mungu aliye hai, tuambie ikiwa wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu.”

Yesu akajibu, “Wewe umenena. 

Lakini ninawaambia nyote, tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu akiwa ameketi mkono wa kuume wa Mwenye Nguvu, na akija juu ya mawingu ya mbinguni.”

Ndipo Kuhani Mkuu akararua nguo zake na kusema, “Amekufuru! Kwa nini tunahitaji ushahidi zaidi? Tazama, sasa ninyi mmesikia hayo makufuru.

Uamuzi wenu ni nini?” Wakajibu, “Anastahili kufa.” "Kisha wakamtemea mate usoni na wengine wakampiga ngumi. Wengine walimpiga makofi na kusema,"

“Tutabirie, wewe Kristo! Ni nani aliyekupiga?” Wakati huu Petro alikuwa amekaa nje uani. Mtumishi mmoja wa kike akamjia na kumwambia, “Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu wa Galilaya.”

Lakini Petro akakana mbele yao wote akisema, “Sijui hilo usemalo.”

LUKE 22

Baadaye kidogo, mtu mwingine alimwona Petro akasema, “Wewe pia ni mmoja wao!” 

Petro akajibu, “Wewe mtu, mimi sio mmoja wao!”

Baada ya muda wa kama saa moja hivi, mtu mwingine akazidi kusisitiza, 

“Kwa hakika huyu mtu naye alikuwa pamoja na Yesu, kwa maana yeye pia ni Mgalilaya.”

Petro akajibu, “Wewe mtu, mimi sijui unalosema!”

Wakati uo huo, akiwa bado anazungumza, jogoo akawika.

Naye Bwana akageuka akamtazama Petro. Ndipo Petro akakumbuka yale maneno ambayo Bwana alimwambia,

“Kabla jogoo hajawika leo, utanikana mara tatu.” Akatoka nje, akalia sana.

MATTHEW 27

Asubuhi na mapema, viongozi wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri pamoja dhidi ya Yesu ili kumwua.

Wakamfunga, wakampeleka na kumkabidhi kwa Pilato, ambaye alikuwa mtawala.

"Yuda, ambaye ndiye aliyekuwa amemsaliti Yesu, alipoona kuwa Yesu amehukumiwa, akajuta na akarudisha vile vipande thelathini vya fedha alivyopewa na viongozi wa makuhani na wazee wa watu.Akasema,"

Nimetenda dhambi, kwa maana nimeisaliti damu isiyo na hatia.”

Basi Yuda akavitupa vile vipande vya fedha ndani ya Hekalu akaondoka 

akaenda kujinyonga.

Wale makuhani wakuu wakazichukua zile fedha wakasema,

“Si halali kuchanganya fedha hizi na sadaka kwa sababu hizi ni fedha zenye damu.”

Kwa hiyo baada ya kushauriana, waliamua kuzitumia kununulia shamba la mfinyanzi, liwe mahali pa kuzikia wageni.

JOHN 18

Ndipo Wayahudi wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa na kumpeleka kwenye jumba la kifalme la mtawala wa Kirumi. Wakati huo ilikuwa ni alfajiri, ili kuepuka kuwa najisi kwa taratibu za ibada, Wayahudi hawakuingia ndani kwa sababu ya sheria za Kiyahudi. Wangehesabiwa kuwa najisi kama wangeingia nyumbani mwa mtu asiye Myahudi na wasingeruhusiwa kushiriki katika Sikukuu ya Pasaka.

Hivyo Pilato akatoka nje walikokuwa akawauliza, 

“Mmeleta mashtaka gani kumhusu mtu huyu?”

Wao wakamjibu, “Kama huyu mtu hakuwa mhalifu tusingemleta kwako.”

Pilato akawaambia, “Basi mchukueni ninyi mkamhukumu kwa kufuata sheria zenu.”

Wayahudi wakamjibu, “Sisi haturuhusiwi kutoa hukumu ya kifo kwa mtu ye yote.”

Walisema hivyo ili yale maneno aliyosema Yesu kuhusu kifo atakachokufa yapate kutimia.

Kwa hiyo Pilato akaingia ndani akamwita Yesu, akamwuliza,

“Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?”

Yesu akamjibu, ‘’Je, unauliza swali hili kutokana na mawazo yako mwenyewe au uliambiwa na watu kunihusu mimi?’’

Pilato akamjibu, ‘’Mimi si Myahudi, ama sivyo?’’ Taifa lako mwenyewe na viongozi wa makuhani wamekukabidhi kwangu. Umefanya kosa gani?’’

Yesu akajibu, “Ufalme wangu si wa ulimwengu huu. Ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu wafuasi wangu wangenipigania ili nisitiwe mikononi mwa Wayahudi. Lakini kama ilivyo ufalme wangu hautoki hapa ulimwenguni.”

Pilato akamwuliza, “Kwa hiyo wewe ni mfalme?” 

Yesu akajibu, “Wewe wasema kwamba mimi ni mfalme. Kwa kusudi hili nilizaliwa na kwa ajili ya hili nilikuja ulimwenguni ili niishuhudie kweli. Mtu ye yote aliye wa kweli husikia sauti yangu.”

Pilato akamwuliza Yesu, “Kweli ni nini?” 

Baada ya kusema haya Pilato akaenda nje tena akawaambia wale viongozi wa Wayahudi waliomshtaki Yesu

“Sioni kosa lo lote alilotenda mtu huyu.

MARK 15

Ilikuwa desturi wakati wa Sikukuu ya Pasaka kumfungulia mfungwa ye yote ambaye watu wangemtaka.

huo, mtu mmoja aitwaye Baraba alikuwa amefungwa gerezani pamoja na waasi wengine waliokuwa wamesababisha mauaji wakati wa maasi yaliyotokea dhidi ya serikali.

Ule umati wa watu ukamjia Pilato na kumwomba awafanyie kama ilivyokuwa desturi yake.

Pilato akawauliza, “Mnataka niwafungulie huyu Mfalme wa Wayahudi?”

maana yeye alitambua kuwa viongozi wa makuhani walikuwa wamemtia Yesu mikononi mwake kwa ajili ya wivu.

Pilato akiwa ameketi kwenye kiti cha hukumu, mkewe akampelekea ujumbe huu: 

“Usiwe na jambo lo lote juu ya mtu huyu asiye na hatia,

kwa kuwa leo nimeteseka sana katika ndoto kwa sababu yake.”

"Lakini viongozi wa makuhani na wazee wakaushawishi ule umati wa watu kwamba waombe Baraba afunguliwe na Yesu auawe.

Mtawala akawauliza tena, " “Ni yupi kati ya hawa wawili mnayetaka niwafungulie?”

Wakajibu, “Baraba.”

JOHN 19

Ndipo Pilato akamtoa Yesu akaamuru apigwe mijeledi.

Askari wakasokota taji ya miiba wakamvika Yesu kichwani. 

Wakamvalisha joho la zambarau.Wakawa wanapanda pale alipo tena na tena, wakisema, 

“Salamu! Mfalme wa Wayahudi!” Huku wakimpiga makofi usoni.

Pilato akatoka tena nje akawaambia wale waliokusanyika,

“Tazameni, namkabidhi Yesu kwenu kuwajulisha kwamba mimi sikumwona ana hatia.”

Kwa hiyo Yesu akatoka nje akiwa amevaa ile taji ya miiba na lile vazi la zambarau. Pilato akawaambia, 

“Tazameni, huyu hapa huyo mtu!” Wale viongozi wa makuhani na maafisa walipomwona, wakapiga kelele wakisema, 

“Msulibishe! Msulibishe!” Pilato akawaambia, “Mchukueni ninyi mkamsulibishe, mimi sioni hatia juu yake.”

Wayahudi wakamjibu, 

“Sisi tunayo sheria na kutokana na sheria hiyo, hana budi kufa kwa sababu yeye alijiita Mwana wa Mungu.”

Pilato aliposikia haya, akaogopa zaidi. Akaingia tena ukumbini akamwuliza Yesu, 

“Wewe umetoka wapi?” Lakini Yesu hakumjibu. Pilato akamwambia, “Wewe unakataa kuongea na mimi? Hujui ya kuwa nina mamlaka ya kukuachia huru au kukusulibisha?”

Ndipo Yesu akamwambia, “Wewe hungekuwa na mamlaka yo yote juu yangu kama hungepewa kutoka juu. Kwa hiyo yeye aliyenitia mikononi mwako ana hatia ya dhambi iliyo kubwa zaidi.”

Tangu wakati huo, Pilato akajitahidi kutafuta njia ya kumfungua Yesu, lakini Wayahudi wakazidi kupiga kelele wakisema,

“Ukimwachia huyu mtu, wewe si rafiki wa Kaisari. Mtu ye yote anayedai kuwa mfalme anampinga Kaisari.”

"Pilato aliposikia maneno haya akamtoa Yesu nje tena akaketi katika kiti chake cha hukumu, mahali palipoitwa Sakafu ya Jiwe, kwa Kiebrania paliitwa Gabatha.Basi ilikuwa siku ya Maandalio ya Pasaka, yapata kama saa sita hivi.Pilato akawaambia Wayahudi, 

“Huyu hapa mfalme wenu!”

MATTHEW 27

Pilato alipoona kwamba hawezi kufanya lo lote, lakini badala yake ghasia zilikuwa zinaanza, akachukua maji, akanawa mikono yake mbele ya ule umati wa watu, akasema,

“Sina hatia juu ya damu ya mtu huyu, hili ni jukumu lenu!”

Watu wote wakajibu, “Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu!”

Basi akawafungulia Baraba na baada ya kumchapa Yesu mijeledi, akamtoa ili asulibiwe.

"Kisha askari wa mtawala wakampeleka Yesu kwenye Praitorio na wakakusanya kikosi kizima cha askari kumzunguka.

Wakamvua nguo zake na kumvika vazi la rangi nyekundu, kishawakasokota taji ya miiba wakaiweka kichwani pake. Wakamwekea fimbo katika mkono wake wa kuume, wakapiga magoti mbele zake na kumdhihaki wakisema "

“salamu, mfalme wa Wayahudi!” Wakamtemea mate, wakachukua ile fimbo wakampiga kichwani tena na tena.

Baada ya kumdhihaki, wakamvua lile vazi, wakamvika tena nguo zake. Kisha wakampeleka ili kumsulibisha.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA MBILI

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadi...

More

Tunapenda kushukuru GNPI-Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha