Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA MBILIMfano

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA MBILI

SIKU 1 YA 7

  MZABIBU NA TAWI

“Mimi ndimi mzabibu wa kweli na Baba yangu ndiye mkulima.

"Kila tawi ndani yangu lisilozaa matunda, Baba yangu hulikata, nalo kila tawi lizaalo, hulisafisha ili lipate kuzaa matunda zaidi.

Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililonena nanyi.Kaeni ndani yangu, nami nikae ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa matunda lisipokaa ndani ya mzabibu, vivyo hivyo ninyi msipokaa ndani yangu hamwezi kuzaa matunda."

“Mimi ni mzabibu, ninyi ni matawi. Akaaye ndani yangu, nami ndani yake, huyo huzaa sana, maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya jambo lo lote.

Mtu ye yote asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka. Matawi kama hayo hukusanywa na kutupwa motoni, yakateketea.

Ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lo lote mtakalo, nanyi mtatendewa.

Kwa hiyo Baba yangu hutukuzwa, kwa vile mzaavyo matunda mengi, nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.

Yesu akatoka akaenda kwenye Mlima wa Mizeituni kama ilivyokuwa kawaida yake, nao wanafunzi wake wakamfuata.

Walipofika huko, akawaambia wanafunzi wake, “Ombeni msije mkaangukia majaribuni.”

Akajitenga nao, kama umbali wa kutupa jiwe, akapiga magoti, akaomba,

akisema, “Baba, kama ni mapenzi yako, niondolee kikombe hiki, lakini si kama mimi nipendavyo, bali mapenzi yako yatendeke.”

Malaika kutoka mbinguni akamtokea, akamtia nguvu.

Naye akiwa katika maumivu makuu, akaomba kwa bidii, nalo jasho lake likawa kama matone ya damu yakidondoka ardhini.

Akarudi kwa wanafunzi wake akawakuta wamelala, naye akamwambia Petro,

“Simoni, umelala? Je, hukuweza kukesha hata kwa saa moja?

Kesheni na kuomba msije mkaingia majaribuni. Roho iko radhi lakini mwili ni dhaifu.”

Akaenda tena kuomba akisema maneno yale yale.

Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA KUMI NA MBILI

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadi...

More

Tunapenda kushukuru GNPI-Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org

Mipangilio yanayo husiana

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha