Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Ishi kwa Nguvu na Ujasiri!Mfano

Ishi kwa Nguvu na Ujasiri!

SIKU 4 YA 8

“Utume wake ni kwa Mtu Binafsi”


Kutoka mwanzo wa uumbaji, Roho Mtakatifu amekuwepo,   akikaa kati yetu kwa vizazi vyote.


“Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa   juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.” Mwanzo 1:2


Lakini ilihitaji mpaka Yesu kukamilisha kazi yake pale   msalabani ndipo huduma ya Roho Mtakatifu kufanyika kuwa binafsi na nafsi ya karibu   sana kwa kila mwamini. Yesu aliwaambia wanafunzi wake kabla hajafa kwamba   Roho Mtakatifu yuko kati kati yao, lakini bado haishi ndani yao.


"Ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea (Roho   Mtakatifu), kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana   anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu. Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu."   Yohana 14:17-18


Ahadi ya Yesu ya faraja kwa wanafunzi wake kabla tu ya   kifo chake ilikuwa kwamba bado atakuwa pamoja nao kiroho, kupitia uwepo wa   Roho Mtakatifu katika maisha yao. Kazi Yesu aliyoanza inaendelea katika   maisha yetu kupitia Roho Mtakatifu. Mungu anamtumia Roho Mtakatifu ndani yetu   kufanya mambo manne:


1.  Anafanya wokovu kuwa halisi kwa mtu.


2.  Anakupa   nguvu za kuishi kwa ushindi.


3.  Anajenga tabia ya Kikristo kukusaidia kukua.


4.  Anafanya mambo yote katika kukupatia mema.

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Ishi kwa Nguvu na Ujasiri!

Hauko peke yako. Uwe na siku 1 au miaka 30 katika imani yako ya Kikristo, ukweli huu unasimama thabiti kwa changamoto zote za maisha. Jifunze jinsi ya kukaribisha msaada wa Mungu kwa ufanisi katika mpango huu. Imechuku...

More

Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha