Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Ishi kwa Nguvu na Ujasiri!Mfano

Ishi kwa Nguvu na Ujasiri!

SIKU 1 YA 8

"Hauko Peke Yako”


Huwa inasemwa kwamba maisha yanahusisha mabonde na milima,   wakati wa kufurahi na ahadi zilizojaa nyakati za changamoto na mashaka.   Maisha sio kupanda kwenda kileleni juu siku zote; isipokuwa ni safari yenye   milima na mabonde. Kila mmoja, waamini na wasioamini kwa pamoja, hupitia   maisha ya kwenda juu na chini.


Lakini kama Wakristo, tuna ahadi ya ajabu toka kwa Mungu   kwamba hatutakabili mabonde ya maisha peke yetu. Haya hapa maneno yake ya   kutia moyo kwetu:


“Iweni hodari na moyo wa ushujaa, msiogope wala msiwahofu;   kwa maana BWANA, Mungu wako, yeye ndiye anayekwenda pamoja nawe,   hatakupungukia wala kukuacha.” Kumbukumbu la Torati 31:6


Ukweli ni kwamba tunahitaji uwepo wa Mungu katika nyakati   zote za changamoto na nyakati za mafanikio. Kwa kujua Mungu yu pamoja nasi,   tunaweza kukabili kila changamoto ya maisha kama ngazi kuelekea mafanikio na   wala sio kushuka kuelekea kukata tamaa.


Hakuna   mlima ulio mkubwa kupita kiasi au bonde lililo chini sana ambalo Mungu   hatakutana nasi. Haijalishi mazingira yanayotukabili, Mungu ni mwaminifu, na   siku zote yuko nasi!

Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Ishi kwa Nguvu na Ujasiri!

Hauko peke yako. Uwe na siku 1 au miaka 30 katika imani yako ya Kikristo, ukweli huu unasimama thabiti kwa changamoto zote za maisha. Jifunze jinsi ya kukaribisha msaada wa Mungu kwa ufanisi katika mpango huu. Imechuku...

More

Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha