Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Uwekezaji Wako Ulio Bora!Mfano

Uwekezaji Wako Ulio Bora!

SIKU 5 YA 5

“Tumia   Kanuni za Ki-Mungu Kila Siku”


“Neno lako   ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.” Zaburi 119:105


Kwa   Wakristo, Neno la Mungu linatoa nguvu ya mwanga katika wakati ambao ni   ulimwengu wa giza. Neno la Mungu litakuwa chanzo hicho cha mwanga kama   tutakuwa wazi kwa kweli zake na kuliruhusu kuzama ndani ya maisha yetu. Yesu   analielezea hili katika mfano unaopatikana katika kitabu cha Mathayo: 


“Akawaambia   mambo mengi kwa mifano, akisema, Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda. Hata   alipokuwa akipanda, mbegu nyingine zilianguka karibu na njia, ndege wakaja   wakazila; nyingine zikaanguka penye miamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara   zikaota, kwa udongo kukosa kina; na jua lilipozuka ziliungua; na kwa kuwa   hazina mizizi zikanyauka. Nyingine zikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea,   ikazisonga; nyingine zikaanguka penye udongo mzuri, zikazaa, moja mia, moja   sitini, moja thelathini.” Mathayo 13:3-8


Mbegu   katika hadithi inawakilisha Biblia, na hali tofauti za udongo zinawakilisha   utayari na uhiari wetu wa kupokea neno la Mungu. Kumbuka kwamba si mbegu zote   zilizopandwa na mkulima zilitoa matokeo aliyoyatarajia, bali ni zile mbegu zilizopandwa kwenye udongo mzuri tu. Soma   Mathayo 13:18-23 kuona ufafanuzi wa Yesu wa simulizi hiyo. Kulima katika   “udongo mzuri” maishani mwetu ina maana tunaruhusu Neno la Mungu kupenya   mawazo yetu na kushawishi shauku na tabia za mioyo yetu. 


“Maana   Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao   wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na   mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya   moyo.” Waebrania 4:12

siku 4

Kuhusu Mpango huu

Uwekezaji Wako Ulio Bora!

Kupata matunda tele na ya baraka huanzia na kufanya uwekezaji ulio sahihi. Kama wewe ni mkristo mpya, hakuna uwekezaji ulio mkuu zaidi unaoweza kufanya katika imani yako zaidi ya kuingiza ndani yako Neno la Mungu mara k...

More

Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha