Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Uwekezaji Wako Ulio Bora!Mfano

Uwekezaji Wako Ulio Bora!

SIKU 1 YA 5

“Uhakika   wa Mapato!”

Katika   ulimwengu wa leo, sentensi hii inafanya mtu astuke na kuleta kushukiwa. Lakini   kuna sheria inayofanya kazi karibu katika kila eneo la maisha: sheria ya   wakati wa kupanda na kuvuna, au kwa maneno rahisi zaidi, “unavuna ulichopanda.”   

Huwezi   kuvuna mavuno mpaka kwanza upande mbegu. Huwezi kupata  mapato mpaka kwanza ufanye uwekezaji. Huwezi   kupata faida ya bidhaa au huduma mpaka kwanza uinunue. Huwezi kuwa na afya   bila ya kula chakula bora na kufanya mazoezi. Kwa mifano yote hii, mapato yanayopatikana   huendana na ubora wa nguvu iliyotolewa kwanza.

Sheria   hiyo hiyo inafanya kazi katika mahusiano yetu na Mungu. Hatuwezi kuvuna   maisha ya mwendo wa utoshelevu na baraka na Mungu mpaka pale tunapokuwa tumepanda mbegu  zitakazotoa mavuno hayo.   Habari njema ni kwamba Mungu ameweka tayari mbegu njema kwa ajili yetu -   inaitwa  Neno Lake,  Biblia. Kupanda kwa ukarimu neno la Mungu   katika maisha yetu hutuhakikishia mapato tele katika uwekezaji huo.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Uwekezaji Wako Ulio Bora!

Kupata matunda tele na ya baraka huanzia na kufanya uwekezaji ulio sahihi. Kama wewe ni mkristo mpya, hakuna uwekezaji ulio mkuu zaidi unaoweza kufanya katika imani yako zaidi ya kuingiza ndani yako Neno la Mungu mara k...

More

Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha