Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kwa nini Pasaka?Mfano

Why Easter?

SIKU 4 YA 5

Uhuru wa nini?



Yesu hayupo tena duniani kimwili, lakini hakutuacha wenyewe. Alimtuma Roho Wake kukaa nasi. Roho Wake anapokuja kukaa ndani yetu, tunapata Uhuru mpya.



Uhuru wa kumjua Mungu



Mambo tunayoyafanya yasiyo sahihi yanatengeneza mpaka kati yetu na Mungu: ‘Dhambi zenu ndizo zinazowatenga na Mungu wenu'. (Isaya 59:2). Yesu alipokufa pale msalabani, aliondoa mpaka uliokuwepo kati yetu na Mungu. Sababu hii, amefanya uwezo wa sisi kuwa na uhusiano na Muumba wetu. Tumekuwa wana wake. Roho anatuhakikishia huu uhusiano, na pia anatusaidia kumjua Mungu zaidi. Anatusaidia kuomba na kuelewa Neno la Mungu (Biblia).



Uhuru wa kupenda



‘Sisi tuna upendo kwa sababu Mungu alitupenda kwanza.’ (1 Yohana 4:19). Tunapoangalia msalaba, tunatambua Upendo wa Mungu juu yetu. Roho wa Mungu anapokuja kuishi ndani yetu, tunapata upendo huo. Vivyo hivyo, tunapata upendo kwa Mungu na wengine. Tunakua huru kuishi maisha yenye upendo- maisha yenye kupenda na kumtumikia Yesu na kupenda na kutumikia wengine kuliko kuishi maisha ya kujijali wenyewe.



Uhuru wa kubadilika



Mara kwa mara watu husema, 'Uko jinsi ulivyo. Huwezi kubadilika.' Habari njema ni kwamba, kupitia msaada wa Roho Mtakatifu, tunaweza kubadilika. Roho Mtakatifu anatupa uhuru wa kuishi aina ya maisha ambayo nafsini mwetu tumetamani kuyaishi. Mt Paulo anatuambia kwamba, tunda la Roho ni 'mapendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili, uaminifu, upole na kuwa na kiasi' (Wagalatia 5:22-23). Pale tunapomwomba Roho Mtakatifu aje na kuishi ndani yetu, mambo makuu yanaanza kujitokeza na kuota ndani ya maisha yetu.


siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Why Easter?

Pasaka ina umuhimu gani? Mbona kuna shauku sana kuhusu mtu aliyezaliwa miaka 2,000 iliyopita? Mbona watu wengi wanachangamka kuhusu Yesu? Kwa nini tunamhitaji? Kwa nini alikuja? Kwa nini alikufa? Kwa nini mtu asumbuke ku...

More

Tungependa kuwashukuru Alpha na Nicky Gumbel kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://alpha.org/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha