Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kwa nini Pasaka?Mfano

Why Easter?

SIKU 1 YA 5

Kwa nini tunamhitaji Yesu?  



Wewe na mimi tuliumbwa ili kuwa katika uhusiano na Mungu. Mpaka tutakapokuwa na uhusiano huo, siku zote kutakuwa na kitu kinachokosekana maishani mwetu. Matokeo yake, mara nyingi tunafahamu kwamba tunapungukiwa. Mwimbaji mmoja analifafanua kwa kusema: ‘Nina utupu ndani yangu.’



Mwanamke mmoja, katika barua, aliniandikia kuhusu ‘utupu wa kina.’ Msichana mwingine alizungumza kuhusu ‘sehemu kubwa inayokosekana nafsini mwake.’



Watu wanajaribu kujaza utupu huu kwa njia tofauti. Wengine wanajaribu kujaza pengo na pesa, lakini hairidhishi. Aristotle Onassis, ambaye alikuwa mojawapo wa matajiri wakubwa
duniani, alisema mwishoni mwa maisha yake: ‘mamilioni hayatoshi kwa kile mwanadamu anachohitaji katika maisha yake.’



Wengine wanajaribu mihadarati ama ulevi ama uzinzi. Msichana mmoja aliniambia, ‘Hivi vitu vinaleta utoshelezo wa papo hapo lakini vinakuacha ukihisi kana kwamba kuna utupu ndani baadaye.’ Wengine wanajaribu kufanya kazi kwa bidii, muziki, michezo ama kutafuta mafanikio. Yamkini hivi vitu si vibaya, lakini havitoshelezi njaa ya kina iliyo ndani ya kila mwanadamu.



Hata uhusiano wa karibu mno wa kibinadamu, ingawa ni mzuri, hauridhishi ‘utupu wa kina wa ndani.’ Hakuna kitu ambacho kitajaza pengo hili ila uhusiano na Mungu ambao tuliumbwa kwa ajili yake.



Kulingana na Agano Jipya, sababu ya utupu huu ni kwamba watu wamemwasi Mungu.



Yesu alisema, ‘Mimi ndimi mkate wa uzima’ (Yohana 6:35). Yeye pekee ndiye anayeweza kuridhisha njaa ya kina kwa sababu yeye ndiye anayewezesha urejesho wa uhusiano wetu na Mungu.



a) Anaridhisha njaa yetu na kusudi maishani



Ni katika uhusiano wetu na muumba wetu ndipo tunapata maana halisi na kusudi la maisha yetu.

b) Hushibisha njaa yetu hata mauti



Watu wengi hawataki kufa. Tunatamani kuishi baada ya kifo. Tunapata uzima wa milele katika Yesu Kristo pekee. 

c)Anashibisha njaa yetu ya msamaha



Tukiwa wakweli, tutakiri kwamba wote tunafanya mambo ambayo tunajua ni makosa. Kwa kifo chake msalabani, Yesu aliwezesha tupate msamaha na kurejeshwa katika uhusiano na Mungu. 

Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Why Easter?

Pasaka ina umuhimu gani? Mbona kuna shauku sana kuhusu mtu aliyezaliwa miaka 2,000 iliyopita? Mbona watu wengi wanachangamka kuhusu Yesu? Kwa nini tunamhitaji? Kwa nini alikuja? Kwa nini alikufa? Kwa nini mtu asumbuke ku...

More

Tungependa kuwashukuru Alpha na Nicky Gumbel kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://alpha.org/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha