Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Injili Ulimwenguni - Sehemu 2Mfano

Injili Ulimwenguni - Sehemu 2

SIKU 7 YA 7

Kukataliwa kwa Yesu Nazareti  

Kisha Yesu akarudi mpaka Galilaya, akiwa amejaa nguvu za Roho Mtakatifu, nazo habari zake zikaenea katika sehemu zote za nchi za kandokando.

Yesu akaenda Nazareti, hapo alipolelewa na siku ya Sabato alikwenda katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake. Akasimama ili asome, naye akapewa kitabu cha nabii Isaya, akakifungua na kukuta mahali palipoandikwa: 

“Roho wa Bwana yu juu yangu,

kwa sababu amenitia mafuta

kuwaletea maskini habari njema.

Amenituma kuwatangazia wafungwa

kufunguliwa kwao na vipofu kupata kuona tena,

kuwaweka huru wanaoonewa

na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubalika.”

Kisha akakifunga kitabu, akamrudishia mtumishi na akaketi. Watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. Ndipo akaanza kwa kuwaambia, “Leo maandiko haya yametimia mkiwa mnasikia.”

Wote waliokuwako wakamsifu na kuyastaajabia maneno yake yaliyojaa neema, wakaulizana, “Je, huyu si mwana wa Yosefu?” Yesu akawaambia, “Bila shaka mtatumia mithali hii, ‘Tabibu, jiponye mwenyewe! Mambo yale tuliyosikia kwamba uliyafanya huko Kapernaumu, yafanye na hapa kwenye mji wako.’”

Yesu akasema, “Amin, nawaambia, hakuna nabii anayekubalika kwenye mji wake mwenyewe.

Lakini ukweli ni kwamba  "palikuwa na wajane wengi katika Israeli wakati wa Eliya, mbingu zilipofungwa kwa miaka mitatu na miezi sita pakawa na njaa kuu katika nchi nzima.

Hata hivyo Eliya hakutumwa hata kwa mmoja wao, bali kwa mjane mmoja wa Sarepta katika nchi ya Sidoni.

"Pia palikuwa na wengi wenye ukoma katika Israeli katika siku za nabii Elisha, lakini hakuna hata mmoja wao aliyetakaswa, isipokuwa Naamani mtu wa Shamu.”

"Watu wote katika sinagogi waliposikia maneno haya, wakakasirika sana. Wakasimama, wakamtoa nje ya mji, wakamchukua hadi kwenye kilele cha mlima mahali ambapo mji huo ulikuwa umejengwa, ili wamtupe chini kutoka kwenye mtelemko mkali.

"Lakini yeye akapita papo hapo katikati ya huo umati wa watu akaenda zake.

siku 6

Kuhusu Mpango huu

Injili Ulimwenguni - Sehemu 2

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadi...

More

Tungependa kumshukuru GNPI Kenya kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org/

 

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha