Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Injili Ulimwenguni - Sehemu 2Mfano

Injili Ulimwenguni - Sehemu 2

SIKU 3 YA 7

Arusi Huko Kana ya Galilaya

Siku ya tatu kulikuwa na arusi katika mji wa Kana ya Galilaya, naye mama yake Yesu alikuwako huko. Yesu pamoja na wanafunzi wake walikuwa wamealikwa arusini pia. Divai ilipokwisha, mama yake Yesu akamwambia, “Wameishiwa na divai.” Yesu akamwambia,  “Mwanamke, nina nini nawe? Saa yangu haijawadia.” Mama yake akawaambia wale watumishi, “Lo lote atakalowaambia, fanyeni.”

Basi ilikuwapo huko mitungi sita ya kuhifadhia maji iliyotengenezwa kwa mawe kwa ajili ya kujitakasa kwa desturi ya Kiyahudi, kila mtungi ungeweza kuchukua vipipa viwili au vitatu.Yesu akawaambia wale watumishi, “Ijazeni hiyo mitungi maji.” Nao wakaijaza ile mitungi mpaka juu. Kisha akawaambia, 

“Sasa choteni hayo maji kidogo, mpelekeeni mkuu wa meza.”

"Hivyo wakachota, wakampelekea.Yule mkuu wa meza akayaonja yale maji ambayo yalikuwa yamebadilika kuwa divai. Hakujua divai hiyo ilikotoka ingawa wale watumishi waliochota yale maji wao walifahamu. Basi akamwita bwana arusi kando akamwambia, 

“Watu wote hutoa kwanza divai nzuri, kisha huleta ile divai hafifu wageni wakisha kunywa vya kutosha, lakini wewe umeiweka ile nzuri kupita zote mpaka sasa.”

Huu, ndio uliokuwa mwujiza wa kwanza Yesu aliofanya huko Kana ya Galilaya. Hivyo Yesu alidhihirisha utukufu wake na wanafunzi wake wakamwamini.

Andiko

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Injili Ulimwenguni - Sehemu 2

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadi...

More

Tungependa kumshukuru GNPI Kenya kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org/

 

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha