Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

TabiaMfano

Habits

SIKU 5 YA 6

Amini Mchakato wa Mungu



Tumekuwa tukiongea mengi kuhusu tabia, lakini ni tabia ni nini, haswa? Kulingana na yale tumejifunza, tabia inaundwa ukiridhisha haja muhimu kila mara na mwenendo fulani. Tabia huwa zina sifa mbaya, lakini ni michakato ambayo Mungu aliumba. Tutaziita michakato ya Mungu. Hii inatuelekeza katika mada ya leo: amini mchakato wa Mungu



Kiini cha kisa cha uumbaji wa Mungu ambacho kimeasimuliwa katika kitabu cha Mwanzo ni tabia njema za kila siku. Hii ni mara ya kwanza ambayo tunaona Mungu akitumia michakato kuunda kitu kipya, bora, na njema. Unatambua haya? Mungu alikuwa na mazoea! Ni hadithi moja tu, lakini Mungu alionyesha tabia za uhodari, kutokata tamaa, kuomba usaidizi kutoka wengine (Adamu aliwapa wanyama majina, Mungu alisema kwamba si vizuri mwanamume kuwa peke yake na akaumba Hawa), kusita ili kusherehekea utendaji wake (Mungu alisema kwamba kazi yake ni vyema kila siku), na kuchukua siku kila wiki kupumzika. Unaposoma Biblia, endelea kutafuta tabia njema, ama michakato ya Mungu, kote, na utagundua kuwa ni zawadi kutoka kwa Mungu. 



Tunafaa kumwamini Mungu na kuamini kwamba Mungu yupo katika mchakato. Anatengeneza kitu kipya na kirembo maishani mwako unapogundua utambulisho bora, unapoomba usaidizi, unapojipa fadhili, unapochunguza na kubadilisha, na kuamini mchakato wake. Michakato kama kukuza tabia njema za kila siku si vitu ambavyo tunatumia ili tusitegemee msaada wa Mungu—bali zipo kwa sababu ya usaidizi wake. Tunapomwamini Mungu na vitendo hivi vya kila siku, zinakuwa michakato yake. Kwa upande mwingine, bila usaidizi wake, jitihada zetu zinakuwa mradi wa kujiokoa. Hii mwelekeo kwamba yote yawezekana bila Mungu ndio uliotuletea shida mwanzoni! 



Omba: Mungu, ninashukuru kwa utaratibu na tabia ambazo unanisaidia kuweka maishani mwangu. Siwezi bila nguvu, amani, na neema yako. Nisaidie kuendelea kukutegemea kila siku. Amina. 


siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Habits

Mabadiliko si rahisi, lakini si kwamba hayawezekani. Kuanza tabia chache rahisi itabadilisha jinsi unajiona leo na kukugeuza uwe mtu ambaye ungependa kuwa kesho. Mpango huu wa Biblia wa Life.Church unatazama Maandiko ili...

More

Tungependa kuwashukuru Life.Church kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tuvuti ya https://www.life.church/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha