Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

TabiaMfano

Habits

SIKU 4 YA 6

Chunguza na Badilisha



Umeanza kuchimba ili kugundua utambulisho bora? Ulibuni malengo yaliyo na msingi wa utambulisho na ukweli ambao unaponya utambulisho kutoka Neno la Mungu? Umepata watu wafaka kuomba usaidizi? Labda umegundua kwamba si rahisi kama ulivyodhani, ama umekosea na tabia yako mpya—lakini ulikumbuka kujipa fadhili. Mada ya leo ni Chunguza na Badilisha.  



Kuchunguza na kubadilisha yana uhusiano upi na chochote? Charles Duhigg, ambaye aliandika Nguvu ya Tabia (The Power of Habit), aliipa dhana ya “kitanzi cha tabia” umaarufu. Kitanzi cha tabia kinahusisha ishara, utaratibu, na zawadi. Ikiwa tabia yake ni kukula kupita kiasi kabla ya kulala, pengine kitanzi ni kama hivi. Ishara: Unaketi na mke/mume wako ama marafiki ili kutazama kipindi na unaona tangazo ambalo lina chakula. Utaratibu: Unaenda kuangalia friji na unapata kitu kitamu. Zawadi: Mwili wako inatoa kemikali chanya unapokula chakula na kuketi na wenzako. Matokeo ni tabia inayojiendeleza. 



Unapovunja tabia ya kale ama kutengeneza mpya, yamkini tutapitia majaribio makali njiani. Wakati mwingine jaribio linatokana na kitanzi cha tabia. Ikiwa unataka kuvunja tabia ya kukula kupita kiaso kabla ya kulala, utataka kuhakikisha kwamba umegundua ishara halisi. Labda si tangazo la chakula, bali kutazama kipindi, kukutana na marafiki, ama vitu vingine vinavyokupa hamu. Aidha, utataka kufikiri kuhusu utaratibu wako. Unaangalia friji kwa sababu ya ukinaifu, ama ni desturi, ama kwa kweli una njaa? Zawadi ni muhimu. Ni chakula chenyewe ama ni kitendo cha kukula na watu wengine ambacho unapenda? Labda una wasiwasi watu fulani wakikuja, ama unakula na kutazama vipindi ili kukwepa mazungumzo ambayo unahitaji kuwa nayo na mume/mke wako. 



Tunapohisi kwamba hatuwezi kuepuka kitanzi cha tabia, tusite, tuchunguze, kisha tubadilishe mambo. Aidha, tutumie kitanzi cha tabia ili kutengeneza tabia njema tukikuza ishara chanya, utaratibu bora, na zawadi zinazofaa. 



Vitabu vingi havitakueleza jambo hili kuhusu kuunda na kuvunja vitanzi vya tabia: Milele pana njia. Tunajuaje? Katika 1 Wakorintho 10:13, Mtume Paulo anatuambia kwamba Mungu ni mwaminifu—hataruhusu tujaribiwe kupita nguvu zetu. Lakini tunapojaribiwa, atatupa njia ya kutoka humo ili tuweze kustahimili. Kwa hivyo tuchunguze, tubadilishe, tumtegemee Mungu, omba usaidizi kutoka watu, na endelea kusonga mbele Mungu akikuongoza.  



Tafakari: Ishara zangu ni zipi? Nitabadilisha aje ishara hasi na chanya? Taratibu zangu zinanipeleka wapi? Ni zawadi zipi zinatokana na tabia zangu? Mambo haya ni yale ambayo Mungu ameniandalia? 


siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Habits

Mabadiliko si rahisi, lakini si kwamba hayawezekani. Kuanza tabia chache rahisi itabadilisha jinsi unajiona leo na kukugeuza uwe mtu ambaye ungependa kuwa kesho. Mpango huu wa Biblia wa Life.Church unatazama Maandiko ili...

More

Tungependa kuwashukuru Life.Church kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tuvuti ya https://www.life.church/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha