Zaburi 77:5-9
Zaburi 77:5-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Nafikiria siku za zamani; nakumbuka miaka ya hapo kale. Usiku nawaza na kuwazua moyoni; natafakari na kujiuliza rohoni: “Je, Bwana ametuacha kabisa? Je, hatatuonesha tena hisani yake? Je fadhili zake zimekoma kabisa? Je, hatatimiza tena ahadi zake? Je, Mungu amesahau kuwa na huruma? Je, hasira yake imeuondoa upole wake?”
Zaburi 77:5-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nilifikiri habari za siku za kale, Miaka ya zamani zilizopita. Nanena na moyo wangu usiku, Nawaza moyoni mwangu, Roho yangu naipeleleza. Je! Bwana atatutupa milele na milele? Asiwe na fadhili kwetu kamwe? Rehema zake zimekoma hata milele? Ahadi yake imekwisha hata vizazi vyote? Mungu amesahau fadhili zake? Amezuia kwa hasira rehema zake?
Zaburi 77:5-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nalifikiri habari za siku za kale, Miaka ya zamani zilizopita. Nakumbuka wimbo wangu usiku, Nawaza moyoni mwangu, Roho yangu ikatafuta. Je! Bwana atatupa milele na milele? Hatatenda fadhili tena kabisa? Rehema zake zimekoma hata milele? Ahadi yake imekwisha hata vizazi vyote? Mungu amesahau fadhili zake? Amezuia kwa hasira rehema zake?
Zaburi 77:5-9 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nilitafakari juu ya siku zilizopita, miaka mingi iliyopita, nilikumbuka nilivyoimba nyimbo usiku. Moyo wangu ulitafakari na roho yangu ikauliza: “Je, Bwana atakataa milele? Je, hatatenda mema tena? Je, upendo wake usio na mwisho umetoweka milele? Je, ahadi yake imekoma nyakati zote? Je, Mungu amesahau kuwa na huruma? Je, katika hasira amezuia huruma yake?”