Zaburi 71:1-3
Zaburi 71:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nimekukimbilia Wewe, BWANA, Nisiaibike milele. Kwa haki yako uniponye, uniopoe, Unitegee sikio lako, uniokoe. Uwe kwangu mwamba wa makazi yangu, Nitakakokwenda sikuzote. Umeamuru niokolewe, Ndiwe genge langu na ngome yangu.
Zaburi 71:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Kwako ee Mwenyezi-Mungu, nakimbilia usalama; kamwe usiniache niaibike! Kwa uadilifu wako uniokoe na kunisalimisha; unitegee sikio lako na kuniokoa! Uwe mwamba wangu wa kukimbilia usalama, ngome imara ya kuniokoa, kwani wewe ni mwamba na ngome yangu.
Zaburi 71:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nimekukimbilia Wewe, BWANA, Nisiaibike milele. Kwa haki yako uniponye, uniponye, Unitegee sikio lako, uniokoe. Uwe kwangu mwamba wa makazi yangu, Ngome imara ya wokovu wangu. Maana wewe, Ndiwe mwamba wangu na ngome yangu.
Zaburi 71:1-3 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ee BWANA, nimekukimbilia wewe, usiache nikaaibika kamwe. Kwa haki yako uniponye na kuniokoa, unitegee sikio lako uniokoe. Uwe kwangu mwamba wa kimbilio, mahali nitakapokimbilia kila wakati; toa amri ya kuniokoa, kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu.