Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 71

71
Sala ya ulinzi wa daima na msaada
1Nimekukimbilia Wewe, BWANA,
Nisiaibike milele.
2Kwa haki yako uniponye, uniponye,
Unitegee sikio lako, uniokoe.
3 # Zab 44:4 Uwe kwangu mwamba wa makazi yangu,
Ngome imara ya wokovu wangu.
Maana wewe,
Ndiwe mwamba wangu na ngome yangu.
4Ee Mungu wangu, uniponye mkononi mwa mkorofi,
Katika mkono wake mwovu na mdhalimu,
5 # Yer 17:7; Rum 15:13 Maana ndiwe tegemeo langu, Ee Bwana MUNGU,
Tumaini langu tokea ujana wangu.
6 # Zab 22:9; Isa 46:3; Yer 3:4 Nimekutegemea Wewe tangu kuzaliwa,
Ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu,
Ninakusifu Wewe daima.
7 # Isa 8:18; Zek 3:8; 1 Kor 4:9 Nimekuwa kifani kwa watu wengi,
Lakini wewe ndiwe kimbilio langu la nguvu.
8Kinywa changu kitajazwa sifa zako,
Na heshima yako mchana kutwa.
9Usinitupe wakati wa uzee,
Nguvu zangu zipungukapo usiniache.
10 # 2 Sam 17:1; Mt 27:1 Kwa maana adui zangu wananiamba,
Nao wanaotaka kuniua hushauriana.
11Wakisema, Mungu amemwacha,
Mfuatieni, mkamateni, hakuna wa kumponya.
12 # Zab 22:11; 35:22; 70:1 Ee Mungu, usiwe mbali nami;
Ee Mungu wangu, fanya haraka kunisaidia.
13 # Zab 35:4; 40:14 Waaibishwe, watoweshwe, adui za nafsi yangu.
Wavikwe laumu na aibu wanaonitakia mabaya.
14Lakini mimi nitakutumainia daima,
Nitaendelea kukusifu zaidi na zaidi.
15 # Zab 35:28; 40:5 Lakini mimi nitakutumainia daima
Na nitaendelea kukusifu zaidi na zaidi.
16 # Zek 10:12; Efe 3:16; Flp 4:13; 2 Tim 2:1 Nitakuja na mambo ya ajabu ya Bwana MUNGU;
Nitawakumbusha watu haki yako Wewe peke yako.
17Ee Mungu, umenifundisha tokea ujana wangu;
Nimekuwa nikitangaza miujiza yako hata leo.
18Na hata nikiwa ni mzee mwenye mvi,
Ee Mungu, usiniache.
Hata niwaeleze watu wa kizazi hiki nguvu zako,
Na kila atakayekuja uweza wako.
19 # Zab 57:10; Mit 24:7; Isa 5:16; Kut 15:11; Zab 35:10; Isa 40:18,25 Na haki yako, Ee Mungu,
Imefika juu sana.
Wewe uliyefanya mambo makuu;
Ee Mungu, ni nani aliye kama Wewe?
20 # Zab 60:3; Hos 6:1 Wewe, uliyetuonesha mateso mengi, mabaya,
Utatuhuisha tena.
Utatupandisha juu tena
Kutoka katika vina virefu chini ya nchi.
21Laiti ungeniongezea ukuu!
Urejee tena na kunifariji moyo.
22 # 2 Fal 19:22; Isa 60:9 Nami nitakushukuru kwa kinanda,
Na kweli yako, Ee Mungu wangu.
Nitakuimbia Wewe kwa kinubi,
Ee Mtakatifu wa Israeli.
23 # Zab 103:4 Midomo yangu itafurahi sana nikuimbiapo,
Na nafsi yangu uliyoikomboa.
24Ulimi wangu nao utasimulia
Haki yako mchana kutwa.
Kwa maana wameaibishwa,
Wametahayarika, wanaonitakia mabaya.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 71: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha