Zaburi 119:166-168
Zaburi 119:166-168 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mwenyezi-Mungu, nakungojea uniokoe; mimi natimiza amri zako. Nazingatia maamuzi yako; nayapenda kwa moyo wote. Nazingatia kanuni na maamuzi yako; wewe wauona mwenendo wangu wote.
Shirikisha
Soma Zaburi 119Zaburi 119:166-168 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA, nimeungojea wokovu wako, Na maagizo yako nimeyatenda. Nafsi yangu imezishika shuhuda zako, Nami nazipenda mno. Nimeyashika mausia yako na shuhuda zako, Maana njia zangu zote ziko mbele zako.
Shirikisha
Soma Zaburi 119