Zaburi 119:118-120
Zaburi 119:118-120 Biblia Habari Njema (BHN)
Unawakataa wote wanaokiuka masharti yako; mawazo yao maovu ni ya bure. Waovu wote wawaona kuwa takataka, kwa hiyo mimi napenda maamuzi yako. Natetemeka kwa kukuogopa wewe; nimejaa hofu kwa sababu ya hukumu zako.
Zaburi 119:118-120 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Umewakataa wote wazikosao amri zako, Kwa maana hila zao ni bure. Wabaya wa nchi pia umewaondoa kama takataka, Ndiyo maana nimezipenda shuhuda zako. Mwili wangu unatetemeka kwa kukucha Wewe, Nami ninaziogopa hukumu zako.
Zaburi 119:118-120 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Umewakataa wote wazikosao amri zako, Kwa maana hila zao ni uongo. Wabaya wa nchi pia umewaondoa kama takataka, Ndiyo maana nimezipenda shuhuda zako. Mwili wangu unatetemeka kwa kukucha Wewe, Nami ninaziogopa hukumu zako.