Zaburi 118:10-12
Zaburi 118:10-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Mataifa yote yalinizingira, lakini kwa jina la Mwenyezi-Mungu nikayaangamiza! Yalinizunguka kila upande, lakini kwa jina la Mwenyezi-Mungu, nikayaangamiza! Yalinizunguka, mengi kama nyuki, lakini yakateketea kama kichaka motoni; kwa jina la Mwenyezi-Mungu niliyaangamiza!
Zaburi 118:10-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mataifa yote walinizunguka; Kwa jina la BWANA niliwakatilia mbali. Walinizunguka, naam, walinizunguka; Kwa jina la BWANA niliwakatilia mbali. Walinizunguka kama nyuki, Walizimika kama moto wa miibani; Kwa jina la BWANA niliwakatilia mbali.
Zaburi 118:10-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mataifa yote walinizunguka; Kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali. Walinizunguka, naam, walinizunguka; Kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali. Walinizunguka kama nyuki, Walizimika kama moto wa miibani; Kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali.
Zaburi 118:10-12 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mataifa yote yalinizunguka, lakini kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali. Walinizunguka pande zote, lakini kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali. Walinizunguka kama kundi la nyuki, lakini walikufa haraka kama miiba iteketeayo; kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali.