Yobu 37:5-7
Yobu 37:5-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Mungu hupiga radi ya ajabu kwa sauti yake, hufanya mambo makuu tusiyoweza kuyaelewa. Huiambia theluji, ‘Anguka juu ya nchi!’ Na manyunyu na mvua, ‘Nyesha kwa nguvu.’ Hufunga shughuli za kila mtu; ili watu wote watambue kazi yake.
Yobu 37:5-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mungu hunguruma kwa kustaajabisha kwa sauti yake; Hufanya mambo makuu, ambayo hatuwezi kuyaelewa. Kwa kuwa huiambia theluji, Anguka juu ya nchi; Na pia kwa manyunyu ya mvua, Hayo manyunyu ya mvua yake nyingi. Huufunga mkono wa kila binadamu; Ili watu wote aliowaumba wajue.
Yobu 37:5-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mungu hunguruma kwa kustaajabisha kwa sauti yake; Hufanya mambo makuu, ambayo hatuwezi kuelewa nayo. Kwani huiambia theluji, Anguka juu ya nchi; Na vivyo manyonyota ya mvua, Na hayo maji ya mvua yake kubwa. Huufunga mkono wa kila binadamu; Ili watu wote aliowaumba wajue.
Yobu 37:5-7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Sauti ya Mungu hunguruma kwa namna za ajabu; yeye hutenda mambo makuu kupita ufahamu wetu. Huiambia theluji, ‘Anguka juu ya dunia,’ nayo manyunyu ya mvua, ‘Uwe mvua ya nguvu.’ Ili wanadamu wote aliowaumba wapate kujua kazi zake, yeye humzuilia kila mtu shughuli zake.