Yobu 36:17-19
Yobu 36:17-19 Biblia Habari Njema (BHN)
“Lakini sasa umehukumiwa kama mwovu, hukumu ya haki imekukumba. Jihadhari ghadhabu isije ikakufanya ukadhihaki, au ukubwa wa mali za kukukomboa ukakupotosha. Je, kilio chako kitafaa kukutoa taabuni, au nguvu zako zote zitakusaidia?
Yobu 36:17-19 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini umejaa hukumu ya waovu; Hukumu na haki hukushika. Basi ujitunze, isije hasira ikakuvuta hata ukafanya mzaha; Wala usikubali ukuu wa ukombozi ukugeuze. Je! Mali yako itatosha, hata usiwe katika taabu, Au uwezo wote wa nguvu zako?
Yobu 36:17-19 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini umejaa hukumu ya waovu; Hukumu na haki hukushika. Basi ujitunze, isije hasira ikakuvuta hata ukafanya mzaha; Wala usikubali ukuu wa ukombozi ukugeuze. Je! Mali yako yatatosha, hata usiwe katika taabu, Au uwezo wote wa nguvu zako?
Yobu 36:17-19 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lakini sasa umelemewa na hukumu kwa ajili ya uovu; hukumu na haki vimekukamata. Uwe mwangalifu ili yeyote asikushawishi kwa utajiri; usipotoshwe kwa fungu kubwa la rushwa. Je, utajiri wako hata nguvu zako nyingi vinaweza kukusaidia usiingie kwenye dhiki?