Yobu 36:15-16
Yobu 36:15-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini Mungu huwaokoa wanyonge kwa unyonge wao hutumia shida zao kuwafumbua macho. Mungu alikuvuta akakutoa taabuni, akakuweka mahali pa wasaa pasipo shida, na mezani pako akakuandalia vinono.
Yobu 36:15-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Yeye humponya aliyetaabika kwa njia ya taabu yake, Na kuyafunua masikio yao kwa maonevu. Naam, yeye angekuongoza utoke katika msiba Hata mahali penye nafasi, ambapo hapana kizuizi; Na kilichowekwa mezani pako kingejaa mafuta.
Yobu 36:15-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Yeye humponya aliyetaabika kwa njia ya taabu yake, Na kuyafunua masikio yao kwa maonevu. Naam, yeye angekuongoza utoke katika msiba Hata mahali penye nafasi, ambapo hapana msonge; Na kilichowekwa mezani pako kingejaa mafuta.
Yobu 36:15-16 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Bali wao wanaoteseka huwaokoa katika mateso yao, na kuzungumza nao katika dhiki zao. “Yeye anakubembeleza utoke katika mataya ya dhiki, ili kukuweka mahali palipo na nafasi mbali na kizuizi, hadi kwenye meza yako ya faraja iliyojaa vyakula vizuri.