Yeremia 23:38-40
Yeremia 23:38-40 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini wao wakivunja amri yangu na kusema, ‘Mzigo wa Mwenyezi-Mungu,’ wakati ambapo mimi niliwakataza wasiseme, ‘Mzigo wa Mwenyezi-Mungu,’ basi, waambie kuwa mimi nitawanyanyua na kuwatupilia mbali, wao wenyewe pamoja na mji niliowapa wao na wazee wao. Nitawaletea fedheha ya milele na aibu ya kudumu ambayo haitasahaulika.”
Yeremia 23:38-40 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini mkisema, Mzigo wa BWANA, basi, BWANA asema hivi, Kwa sababu mwasema neno hili, “Mzigo wa BWANA”; nami nimemtuma mtu kwenu kusema, Msiseme, “Mzigo wa BWANA”; basi, kwa hiyo angalieni, nitawasahau ninyi kabisa, nami nitawatupilia mbali, pamoja na mji huu niliowapa ninyi na baba zenu, mtoke mbele za uso wangu; nami nitaleta juu yenu aibu ya milele, na fedheha ya daima, ambayo haitasahauliwa.
Yeremia 23:38-40 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini mkisema, Mzigo wa BWANA, basi, BWANA asema hivi, Kwa sababu mwasema neno hili, “Mzigo wa BWANA”; nami nimemtuma mtu kwenu kusema, Msiseme, “Mzigo wa BWANA”; basi, kwa hiyo angalieni, nitawasahau ninyi kabisa, nami nitawatupilia mbali, pamoja na mji huu niliowapa ninyi na baba zenu, mtoke mbele za uso wangu; nami nitaleta juu yenu aibu ya milele, na fedheha ya daima, ambayo haitasahauliwa.
Yeremia 23:38-40 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ingawa unadai, ‘Huu ndio mzigo wa BWANA,’ hili ndilo BWANA asemalo: Ulitumia maneno, ‘Huu ndio mzigo wa BWANA,’ hata ingawa nilikuambia kuwa kamwe usiseme, ‘Huu ni mzigo wa BWANA.’ Kwa hiyo, hakika nitakusahau na kukutupa mbali na uso wangu pamoja na mji niliowapa ninyi na baba zenu. Nitaleta juu yako fedheha ya kudumu: yaani aibu ya kudumu ambayo haitasahaulika.”