Hosea 6:7-9
Hosea 6:7-9 Biblia Habari Njema (BHN)
“Lakini mlilivunja agano langu kama mlivyofanya mjini Adamu; huko walinikosea uaminifu. Gileadi ni mji wa waovu, umetapakaa damu. Kama wanyang'anyi wamwoteavyo mtu njiani, ndivyo na makuhani walivyojikusanya na kuvizia. Wanaua watu njiani kuelekea Shekemu, naam, wanatenda uovu kupindukia.
Hosea 6:7-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini wao wamelivunja hilo agano kama Adamu; huko wamenitenda mambo ya hiana. Gileadi ni mji wa hao watendao maovu, umetiwa rangi ya damu. Na kama vile makundi ya wanyang'anyi wamwoteavyo mtu, ndivyo kundi la makuhani wauavyo katika njia ielekeayo Shekemu; naam, wametenda mambo maovu sana.
Hosea 6:7-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini wao wamelivunja hilo agano kama Adamu; huko wamenitenda mambo ya hiana. Gileadi ni mji wa hao watendao maovu, umetiwa rangi ya damu. Na kama vile makundi ya wanyang’anyi wamwoteavyo mtu, ndivyo kundi la makuhani wauavyo katika njia ielekeayo Shekemu; naam, wametenda mambo maovu sana.
Hosea 6:7-9 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wamevunja Agano kama Adamu: huko hawakuwa waaminifu kwangu. Gileadi ni mji wenye watu waovu, umetiwa madoa kwa nyayo za damu. Kama wanyangʼanyi wamviziavyo mtu, ndivyo magenge ya makuhani wafanyavyo; wanaulia watu kwenye njia iendayo Shekemu, wakifanya uhalifu wa aibu.