Waebrania 3:3-4
Waebrania 3:3-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini Yesu anastahili heshima kubwa kuliko Mose maana mjenzi wa nyumba hupata heshima zaidi kuliko hiyo nyumba yenyewe. Kila nyumba hujengwa na mtu fulani, lakini Mungu ndiye mjenzi wa vitu vyote.
Waebrania 3:3-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa maana huyo amehesabiwa kuwa amestahili utukufu zaidi kuliko Musa, kama vile yeye aitengenezaye nyumba alivyo na heshima zaidi ya hiyo nyumba. Maana kila nyumba imetengenezwa na mtu; ila yeye aliyevitengeneza vitu vyote ni Mungu.
Waebrania 3:3-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)