Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waraka kwa Waebrania 3

3
Musa ni mtumishi, Kristo ni Mwana
1 # Ebr 4:14 Kwa hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu, Yesu, 2#Hes 12:7 aliyekuwa mwaminifu kwake yeye aliyemweka, kama Musa naye alivyokuwa, katika nyumba yote ya Mungu. 3Kwa maana huyo amehesabiwa kuwa amestahili utukufu zaidi kuliko Musa, kama vile yeye aitengenezaye nyumba alivyo na heshima zaidi ya hiyo nyumba. 4Maana kila nyumba imetengenezwa na mtu; ila yeye aliyevitengeneza vitu vyote ni Mungu. 5#Hes 12:7 Na Musa kweli alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu kama mtumishi, awe ushuhuda wa mambo yatakayonenwa baadaye; 6#Efe 2:19; Kol 1:23 bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba ya Mungu; ambaye nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na fahari ya tumaini letu mpaka mwisho.
Onyo juu ya kutoamini
7 # Zab 95:7-11 Kwa hiyo, kama anenavyo Roho Mtakatifu,
Leo, kama mkisikia sauti yake,
8 # Kut 17:7; Hes 20:2-5 Msifanye mioyo yenu kuwa migumu,
Kama wakati wa kuasi,
Siku ya kujaribiwa katika jangwa,
9Hapo baba zenu waliponijaribu, wakanipima,
Wakaona matendo yangu miaka arubaini.
10Kwa hiyo nilichukizwa na kizazi hiki,
Nikasema, Sikuzote ni watu waliopotoka mioyo hawa;
Hawakuzijua njia zangu;
11 # Hes 14:21-23 Kama nilivyoapa kwa hasira yangu,
Hawataingia rahani mwangu.
12Hadharini, ndugu zangu, usiwepo katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutoamini, ujitengao na Mungu aliye hai. 13#1 The 5:11 Lakini mwonyane kila siku, maadamu inaitwa leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi. 14#Ebr 6:11; 11:1 Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho; 15#Zab 95:7-8 kama inenwavyo,
Leo, kama mkisikia sauti yake,
Msifanye mioyo yenu kuwa migumu,
Kama wakati wa kuasi.
16 # Hes 14:1-35; Kut 17:1 Maana ni akina nani walioasi, waliposikia? Si wale wote waliotoka Misri wakiongozwa na Musa? 17#Hes 14:29; 1 Kor 10:10 Tena ni akina nani aliochukizwa nao miaka arubaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa? 18#Hes 14:22,23 Tena ni akina nani aliowaapia ya kwamba hawataingia katika pumziko lake, ila wale walioasi? 19Basi twaona ya kuwa hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutoamini kwao.

Iliyochaguliwa sasa

Waraka kwa Waebrania 3: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha