Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ebr 3

3
Musa ni Mtumishi, Kristo ni Mwana
1 # Ebr 4:14 Kwa hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu, Yesu, 2#Hes 12:7aliyekuwa mwaminifu kwake yeye aliyemweka, kama Musa naye alivyokuwa, katika nyumba yote ya Mungu. 3Kwa maana huyo amehesabiwa kuwa amestahili utukufu zaidi kuliko Musa, kama vile yeye aitengenezaye nyumba alivyo na heshima zaidi ya hiyo nyumba. 4Maana kila nyumba imetengenezwa na mtu; ila yeye aliyevitengeneza vitu vyote ni Mungu. 5#Hes 12:7Na Musa kweli alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu kama mtumishi, awe ushuhuda wa mambo yatakayonenwa baadaye; 6#Efe 2:19; Kol 1:23bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba ya Mungu; ambaye nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na fahari ya taraja letu mpaka mwisho.
Onyo dhidi ya Kutoamini
7 # Zab 95:7-11 Kwa hiyo, kama anenavyo Roho Mtakatifu,
Leo, kama mtaisikia sauti yake,
8 # Kut 17:7; Hes 20:2-5 Msifanye migumu mioyo yenu,
Kama wakati wa kukasirisha,
Siku ya kujaribiwa katika jangwa,
9Hapo baba zenu waliponijaribu, wakanipima,
Wakaona matendo yangu miaka arobaini.
10Kwa hiyo nalichukizwa na kizazi hiki,
Nikasema, Sikuzote ni watu waliopotoka mioyo hawa;
Hawakuzijua njia zangu;
11 # Hes 14:21-23 Kama nilivyoapa kwa hasira yangu,
Hawataingia rahani mwangu.
12Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hai. 13#1 The 5:11Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi. 14#Ebr 6:11; 11:1Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho; 15#Zab 95:7-8hapo inenwapo,
Leo, kama mtaisikia sauti yake,
Msifanye migumu mioyo yenu,
Kama wakati wa kukasirisha.
16 # Hes 14:1-35; Kut 17:1 Maana ni akina nani waliokasirisha, waliposikia? Si wale wote waliotoka Misri wakiongozwa na Musa? 17#Hes 14:29; 1 Kor 10:10Tena ni akina nani aliochukizwa nao miaka arobaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa? 18#Hes 14:22,23Tena ni akina nani aliowaapia ya kwamba hawataingia katika raha yake, ila wale walioasi? 19Basi twaona ya kuwa hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao.

Iliyochaguliwa sasa

Ebr 3: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha