Waebrania 3:17-19
Waebrania 3:17-19 Biblia Habari Njema (BHN)
Mungu aliwakasirikia akina nani kwa miaka arubaini? Aliwakasirikia wale waliotenda dhambi, maiti zao zikatapakaa kule jangwani. Mungu alipoapa: “Hawataingia mahali pangu pa pumziko,” alikuwa anawasema akina nani? Alikuwa anasema juu ya hao walioasi. Basi, twaona kwamba hawakuingia huko kwa sababu hawakuamini.
Waebrania 3:17-19 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tena ni akina nani aliochukizwa nao miaka arubaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa? Tena ni akina nani aliowaapia ya kwamba hawataingia katika pumziko lake, ila wale walioasi? Basi twaona ya kuwa hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutoamini kwao.
Waebrania 3:17-19 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tena ni akina nani aliochukizwa nao miaka arobaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa? Tena ni akina nani aliowaapia ya kwamba hawataingia katika raha yake, ila wale walioasi? Basi twaona ya kuwa hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao.
Waebrania 3:17-19 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lakini ni nani aliowakasirikia miaka arobaini? Je, si wale waliofanya dhambi ambao miili yao ilianguka jangwani? Ni nani hao ambao Mungu aliapa kuwa kamwe hawataingia rahani mwake isipokuwa ni wale waliokataa kutii? Hivyo tunaona kwamba hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao.